TUJIKUMBUSHEEE KIDOGO
GOLOSO LA SOKA
NA YOSSIMA SITTA,
0769-183981
WAJUMBE TFF WAMETAKA
MABADILIKO
-Kila ukisikia kuna uchaguzi puresha na homa huwa zinapanda
kwa wangombea na wapenzi wake kukiwa na wagombea wote wanaokubalika kwenye
jamii. Huwa tunashudia chaguzi nyingi za siasa za CCM na CHADEMA, wakipigana
vikumbo kumpata muwakilishi wake. Wajumbe wa TFF na GOLOSO walifanya kweli
kuchagua viongozi wake kwani wamechagua mabadiliko. Wajumbe wa kolamu hii ya
goloso walichagua viongozi wao wa Goloso(g9) katika nafasi za mwenyekiti,
katibu na mhasibu. Ama kweli wajumbe wa goloso (wazee wa ting) walichagua
mabadiliko Attu Gervas(Cahil) aliibuka kidedea kuwa mwenyekiti kwa kuwashida
wenzake Kway Yudathadei(Vidic), Erick Gwakisa (Evra) huku nafasi ya katibu
ikienda kwa kiungo matata Rajabu Juma(Wilshere) na kuwashida Danny Justine
(Chicharito) na Lukuba Endrew (Januzaj). Mshambuliaji ambaye mkataba wake
unaelekea ukingoni Lewandowski (Masala Yohana) aliibuka kuwa mhasibu na msemaji
wa Goloso na kuwaacha kwa mbali sana Ngully Alex (Mata) na Molla Jerome (Cech).
-Narudi kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF waliomchagua
mwenyekiti mpya Jamal Malinzi kuwa rais mpya wa TFF kwa kura 73 dhidi ya
mpinzani wake pekee Athuman Jumanne Nyamlani aliyepata kula 52. Huku nafasi ya
makamu wa Rais ikienda kwa Wallace Peter Karia aliyepata kura 67 na kuwashida
Ramadhani Omari Nassibu kura 52 huku Iman Madega akipata kura 6. Wajumbe
walichoshwa na mizengwe ya TFF na kuamua kuchagua mabadiliko. Namkumbuka ndugu
yangu Michael Wambura huwa anawekewa pingaminzi kila chaguzi ambaye uchaguzi wa
kwanza ulisitishwa baada ya yeye na Rais mpya wa TFF kuenguliwa kwenye
uchanguzi. Naamin angekuwepo kwenye uchaguzi huu angeibuka kidedea naye maana
wajumbe wa mkutao mkuu wa TFF walichoshwa na mizengwe iliyokuwa inaendelea
ndani na nje ya TFF na kuamua kuchangua mabadiliko.
-Jamal malinzi nilimnukuu akisema, “nawashukuru wajumbe wa
mkutano mkuu wa TFF kwa kunikubali na kunichagua mimi jamal malinzi niwe rais
wa TFF, ama kweli dunia imekuwa kijiji kwani ndani ya masaa 72 baada ya
kuzindua ilani ya uchaguzi nimepokea
salamu, maoni na mapendekezo toka ndani na nje ya Tanzania ikiwa pamoja ni
Burundi, Ivory Coast, Denmark na NewZealand hatimaye tumechagua mabadiliko”
mwisho wa kunukuu.
-Nilisoma vizuri sera na ilani za viongozi wote wawili
Nyamlani na Malinzi sikuona kosa kwa wajumbe wa mkutano wa TFF kuchagua
mabadiliko. Imebaki kazi ya Rais mpya kutekeleza ilani yake alianza kwa kutoa
msamaha kwa watu wote waliokuwa wamefungiwa kuanzia ngazi ya wilaya , mkoa na
TFF lakini msamaha huo hauwahusu wale waliofungiwa kwa makosa ya rushwa na
kupanga matokeo , pia msamaha huo hauhusu adhabu zilizotolewa katika ngazi ya
klabu. Ni kazi nzuri Rais wa mabadiliko.
-Wajumbe wakaenda mbali sana wakiwa wanataka kuchagua
mabadiliko. Kanda ya soka la Tanzania wakamchangua mpiganaji Kidao Wilfred
Mzigama kuwakilisha kanda ya 13 Dar es Salaam. Kidao alihangaika sana kwenye
kamati kuvuka ila dakika za mwisho mwisho akavuka na jamaa yake Shaffih Dauda
akatupwa nje. Mwisho wa siku wajumbe wakachagua mabadiliko.
-Rais aliyemaliza muda wake leodegar tenga tangu 2004 mpaka
2013 ameacha mazuri na mabaya, imebaki kazi ya Jamal malinzi kuyaacha ya akina
Agape Fue na kuendeleza mazuri yaliyoachwa na tenga .Pia kuyaacha mabaya yote
ya akina Tenga, Nyamulani na timu yake.
mwandishi wa makala hii ni yocma sitta mhariri wa goloso
makala hii ilikuwa ya wakati wa uchaguzi wa TFF
0 comments:
Post a Comment