Pages

Monday, 10 March 2014

RATIBA YA UEFA Champions League



Leo, Jumanne (11.03.2014)

22:45 Bayern München vs Arsenal

22:45 Atlético Madrid vs Milan ...

Kesho, Jumatano (12.03.2014)


22:45 Barcelona vs Manchester City


22:45 PSG vs Bayer Leverkusen

Sunday, 9 March 2014

YANGA YAFA KIUME MISRI

Baada ya al ahly kuogoza kwa bao moja kwa bila ndai ya dak 90.
ndio hatua ya kupigiana penati ukafuata na matokeao ni kama ifuatavyo
Al Ahly wamepata penati 4 - 3 Young Africans
Waliopata Yanga Didier, Canavaro, Okwi huku waliokosa ni Oscar, Bahanuzi na Twite
Al ahly wanafuzu hatua ya 16 bora

PICHA YA SIKU


NANI KAMA DAVID MOYES….????


             GOLOSO LA SOKA

          Na yudathadei kway
                   0768-154424
Nianze kwa kuwasabahi, kila mdau kwa nafasi yake.Ni kwa mara nyingine tunakutana hapa kijiweni katika dawati hili la michezo na burudani tukijaribu kuumiza bongo zetu.Basi leo ninakuja na mada ya moto kati ya mada za moto  nje ya mipaka ya nchi yetu hususani katika Bara la Ulaya,bara linaloonekana kua na mvuto zaidi katika tasnia hii ya soka na zaidi tukijikita katika viunga vya jiji la Manchester katika klabu kongwe ya Manchester United FC.

Klabu hii ilianzishwa hapo mwaka 1878 na kuitwa Newton Heath LYR Football Club na mnamo mwaka 1902 jina likabadilishwa na kuwa Manchester United.Klabu hii imekua na mafanikio makubwa chini ya makocha mbalimbali wakiwa wameharibu rekodi zilizowekwa na makocha wengine lakini pia wakiweka na wengine kuvunja rekodi katika klabu hii kongwe.

Leo hii ni katika kumuangazia kocha wa sasa David Moyes aliye rithi mkoba ya babu Sir Alex Ferguson.Moyes amekua na wakati mgumu sana kiujumla katika klabu hii ya Greater Manchester na hii imechochewa na sababu mbalimbali kulingana na mitazamo na maono ya wadau tofautitofauti.Katika kupunguza ukosefu wa vithibitisho,basi tujaribu kuzitazama rekodi mbalimbali alizoweka kwa kuharibu za zamani lakini pia tuziangalie zilezilizovunjwa na meneja huyu

Rekodi ya kwanza kuwekwa na kocha huyu ni ile ya kuwa kocha wa kwanza kabisa kuanza majukumu yake na kubeba kikombe,Ilikua mnamo tarehe 11 mwezi wa nane ambapo magoli mawili ya mpachika magoli mahiri Robin Van Persie alipowatungua Wigan magoli mawili bila na kuiwezesha klabu yake kutwaa  ngao ya hisani.

Rekodi nyingne ni ile iliyowekwa na klabu hii chini ya kocha wake huyu ya kushinda mechi yake ya kwanza ya ligi kuu nchini uingereza tokea mwaka 1977 timu hii ilipokuwa chini ya kocha Dave Sexton. Rekodi hii iliwekwa katika dimba la Liberty Stadium likitazamwa na mashabiki wapatao 20,733 kwa Manchester United kuichabanga Swansea magoli manne kwa moja.

Lakini pia kocha huyu ameiwezesha klabu hii kupata ushindi mnono ugenini katika makombe yanayo shirikisha vilabu vya Ulaya tokea hapo mwaka 1957 ambapo kocha Busly Babes alipoiadhibu Ireland’s Shamrock Rovers kwa magoli sita bila.Moyes amekuja kukumbushia hayo kwa kuiongoza timu yake kuilabua klabu ya nchini ujerumani,Bayer Leverkusen kwa magoli matano bila hapo tarehe 27 ya mwezi wa kumi na moja

Kocha huyu pia ameweza kuvunja rekodi zilizowekwa na makochawengine katika klabu hii kwa kumsainisha mkataba mnono katika klabu hio na hata katika klabu nyingine zote katika ligi kuu ya Uingereza mchezaji wake Wayne Rooney.Mchezaji huyo raia wa uingereza amesaini mkataba wa kumfunga klabuni hapo kwa miaka mitano na nusu akiwa analipwa paundi 300000 kwa wiki na katika kipindi chote cha mkataba kusadikika kupata paundi milioni 85.

Rekodi nyingine aliyowekwa ni ile ya kumsajili kiungo mshambuliaji Juan Mata kutoka katika klabu ya Chelsea FC kwa kitita cha paundi milioni 37.1 na kuvunja rekodi ya uhamisho klabuni hapo mnamo mwaka 2008 kwa Sir Alex kumsajili kutoka Totenham mchezaji Dimitar Berbatov kwa kitita cha paundi milioni 30.75.Ikiunganishwa na uhamisho wa kiungo mkabaji Marouane Fellaini kutoka Everton katika majira ya joto ulioighaimu klabu ya Man U paundi milioni 27.5,David Moyes anaweka rekodi nyingine kwa kutumia kiasi kikubwa kabisa cha pesa katika msimu mmoja kipatacho paundi milioni 64.6.

Kocha huyu pia ameweza kuweka rekodi mbovu klabuni hapo katika msimu wake wa kwanza katika kuinoa klabu hii na kua katika ya vigezo hasi kwa wadau wa soka mpaka kuanza kuutilia mashaka ufanisi wake wa kazi kulinganisha na makocha wengine,rekodi hizi ziko hapa chini katika mapana yake

Mpaka sasaivi klabu hii kongwe imefungwa mechi zipatazo nane katika ligi kuu na bado ikiwa na kibarua kikubwa katika mechi za usoni.Tukirejea karika historia ya klabu hii inaonekana katika misimu miwili,ya 2001-2002 na 2003-2004 klabu hii ilipoteza mechi tisa kila msimu lakini bado ilimaliza ikiwa nafasi ya tatu katika kila msimu.Tusubiri mpaka mwisho wa msimuilituone  itakuaje.

Rekodi nyingine mbaya kwa kocha huyu ni ile ya Manchester city FC kuiadhibu man U magoli manne kwa moja katika dimba la Etihad.Kwa mara ya mwisho ilitokea katika dimba hilohilo mnamo mwaka wa 1989 ambapo Man U waliadhibiwa vikali kwa magoli matano kwa moja.

Kuthibitisha ni jinsi gani mpaka timu ndogo kimafanikio zinavojizolea sifa kutoka kwa mashabiki wao na hata kuwapa mashabiki wa timu pinzani na man U kupata mwanya wa kuiogelea vibaya timu hii,Klabu ya Stoke City,the potters imefanikiwa kuichachatya man U katika msimu huu,mara yao ya mwisho ikiwa ni mwaka 1984.

Lakini pia Newcastle United kupitia mshambuliaji wake Yohan Cabaye,imeweza kukata kiu yake ya miaka 41 bila kuifunga Manchester united katika dimba la Old Trafford.Katika mechi zipatazo 32 man U wamekua wakiibuka washindi lakini Cabaye aliweza kuharibu rekodi hii chini ya kocha David Moyes.

Katika michuano ya vilabu barani ulaya,David Moyes amezidi kujiharibia sifa klabuni hapo kwa kipigo cha mbili bila kutoka kwa klabu ya Olympiakos katika hatua ya 16 bora na hivyo  kuwa klabu ya kwanza ya ugiriki kuifunga Man U katika hatua hii.

Katika kuhitimisha,sitaki kutoa tamko lolote kumhusu David Moyes kwani nahisi bado ni mapema sana kulingana na uhalisia wa klabu ya Man U kwa makocha wake kihistoria.Lakusema hapa ni moja tu kulingana na uhalisia wa soka,iwe timu ya klabu au timu ya taifa,’’Soka ni sawa na mashua baharini,mawimbi yakitanda mashua hupata wakati mgumu katika safari yake  mithiri ya tumbo kuvurugika na mawimbi yakitulia hali hua shwari’’.Tukutane kijiweni wakati mwingine wadau,Hili ndilo dawati la soka bhana.

mwadishi wa makala hii ni msanifu wa habari za kimataifa wa goloso

Friday, 7 March 2014

PICHA YA SIKU


BODI YA LIGI YATOA ADHABU YA FAINI KWA :


Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeipiga faini ya jumla ya sh. milioni 1/- klabu ya Simba kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo vitendo vinavyoashiria kuwa timu hiyo inaendekeza ushirikina uwanjani.

Klabu ya Simba inasemekana kufanya vitendo hivyo katika mechi yake dhidi ya Mbeya City ambapo imepigwa faini ya sh. 500,000/- na faini nyingine ya sh. 500,000/- wamepigwa makocha wake Loga, Selemani Matola na Idd Pazi kwa kuingia uwanjani na kumzonga mwamuzi kwenye mechi hiyo.

Naye mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe amepigwa faini ya sh. 500,000/- kwa kushangilia bao alilofunga kwenye mechi hiyo kwa kuonesha ishara ya matusi kwa kidole.

Pia Mbeya City imepigwa faini ya sh. 300,000/- kwa kitendo cha washabiki wake kuingia uwanjani kwenye mechi dhidi ya Kagera Sugar iliyochezwa mjini Bukoba. Nazo klabu za Yanga na Coastal Union zimepigwa faini ya sh. 500,000/- kila moja kwa washabiki wao kurusha chupa za maji uwanjani wakati timu hizo zilipopambana jijini Tanga.

Kiungo wa Mtibwa Sugar, Shabani Nditi amepigwa faini ya sh. 500,000/- kwa kumpiga mchezaji wa Simba, wakati Salvatory Ntebe pia wa Mtibwa Sugar amepigwa faini ya sh. 500,000/- kwa kumtukana refa kwenye mechi dhidi ya Mbeya City.

Pia mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Musa Mgosi amepigwa faini ya sh. 500,000/- kwa kosa la kupigana uwanjani kwenye mechi dhidi ya Ashanti United ambapo vilevile atakosa mechi tatu za ligi. Coastal Union imepigwa faini ya sh. 500,000/- kwa washabiki wake kumrushia chupa za maji kipa wa Mbeya City.

Nayo JKT Ruvu imepigwa faini ya sh. 300,000/- kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi dhidi ya Simba iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

RATIBA - Jumamosi, March 8 (England - Premier League)





15:45 West Bromwich Albion vs Manchester United ...

18:00 Cardiff City vs Fulham


18:00 Crystal Palace vs Southampton


18:00 Norwich City vs Stoke City


20:30 Chelsea vs Tottenham Hotspur

Thursday, 6 March 2014

YANGA YAHAMISHWA UWANJA, SASA KUSAFIRI MASAA MAWILI KWENDA MJI WA ALEXANDRIA.


Baada ya ukimya na utata, sasa imetangazwa kuwa mechi kati ya mabingwa Afrika, Al Ahly na wale wa Tanzania Bara, Yanga itapigwa kwenye Uwanja wa Max mjini Alexandria.
Mji huo uko kwenye pwani ya bahari ya Mediterranean, kilomita zaidi ya 200 kutoka katika jiji hili la Cairo, mwendo wa zaidi ya masaa mawili.
Awali ilikuwa siri, lakini leo mchana  kiongozi wa umoja wa klabu za Misri, Tharwat Swelam ameviambia vyombo vya habari mechi hiyo itapigwa bila ya mashabiki.
“Lakini muda utakuwa ni saa moja usiku (saa mbili Bongo) kama ilivyopangwa awali, pia hatutaruhusu mashabiki,” alisema.
Kutokana na uamuzi huo, Yanga sasa inalazimika kusafiri tena kwenda Alexandria na bado uongozi wake haujatoa msimamo wake.
Awali uongozi wa Yanga ulisema kama mechi itachezwa Alexandria basi lazima wapewe ndege,
“Mechi ikibadilishwa baada ya siku tatu kabla ya siku iliyopangwa hakuna tatizo kwa sheria za Caf na pake Alexandiria si mbali,” alisema Mohamed Mowad ambaye ni mkurugenzi wa masuala ya habari.
Suala hilo lilikuwa na utata mkubwa, lakini mwisho limefikia hapo na ainaonekana Al Ahly wana hofu ya kufanyiwa fujo na mashabiki wao iwapo watapoteza mchezo huo.
Lakini Watanzania wanaoishi hapa wanasema hizo ni mbinu za kuwavuruga Yanga ili wazidi kuchanganyikiwa.
Baadaye jioni, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema amepata taarifa hizo na tayari analifanyia kazi.
"Kweli tumepata taarifa hizo na tayari tumeanza kulifanyia kazi suala hilo," alisema Sanga.

MSIMAMO WA LIGI KUU MPAKA SASA

#   Team MP W D L F A D P t
1 18 11 7 0 35 12 +23 40

2 17 11 5 1 41 12 +29 38

3 20 9 9 2 24 16 +8 36

4 20 9 8 3 38 21 +17 35

5 Previous rank: 6 20 7 8 5 18 16 +2 29

6 Previous rank: 7 19 5 10 4 14 9 +5 25

7 Previous rank: 8 19 6 7 6 23 23 +0 25

8 Previous rank: 5 20 6 7 7 22 29 -7 25

9 Previous rank: 10 20 7 1 12 16 30 -14 22

10 Previous rank: 9 19 4 9 6 19 20 -1 21

11 Previous rank: 13 20 4 6 10 12 29 -17 18

12 Previous rank: 11 20 4 5 11 16 34 -18 17

13 Previous rank: 12 20 2 9 9 14 29 -15 15

14 20 2 7 11 12 24 -12 13

ARSENAL FC YA LEO NA ILE TUNAYOITARAJIA


                         GOLOSO LA SOKA 
Na  Kway Yudathadei

Arsenal ni kati ya klabu kubwa,maarufu,yenye uwezo kifedha  na zaidi yenye mashabiki lukuki katika kona mbali za sayari hii ya Dunia nisijue zaidi hata nje ya mipaka ya dunia hii.Ni mengi yanaweza kuzungumziwa kuhusu klabu hii lakini nitapenda kuyaweka hadharani katika dawati hili la soka machache  tu ninayohisi yataweza kuwagusa wadau .
Klabu hii ni ya mpira wa miguu(soka) yenye maskani yake katika  eneo liitwalo Holloway huko kusini mwa Jiji la London na ilianzishwa mnamo mwaka 1886 japokua mafanikio yake yalianza kuonekana zaidi katika miaka ya 1930.
Katika kuitazama Arsenal ya  kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2014 yako machache ya kusemea.Klabu hii imeweza kupata mataji mawili tu ya ligi kuu ya nchini Uingereza na mataji hayo yalipatikana katika misimu ya 2001/2002 na 2003/2004.Hizi ni enzi ambazo Arsenal FC waliweza kuijulisha dunia ni kwa jinsi gani wanaweza kulitandaza soka sio tu kuishia kupiga pasi zenye macho ila hata kupachika mabao na kuzuia wapinzani wao kupitia mabeki mahiri kabisa waliokuwa nao enzi hizo.
Arsene Wenger ni kocha aliye kabidhiwa majukumu ya kuinoa timu hio katika mwaka 1996 na alidhihirisha ubora wake  kwani ukiachana na kuchukua kombe la ligi kuu miaka miwili baada ya yeye kuanza kuinoa timu hio na hata kufanya usajili wenye manufaa kwa kuwanunua wachezaji makini kama Patrick Vieira,Emmanuel Petit,Marc Overmars,Nicolas Anelka na  wengineo wengi,mwaka 2000 aliiwezesha timu hio kufika katika hatua ya Fainali ya kombe la mabingwabarani Ulaya,aliendeleza ubabe kwa kuchukua kombe la ligi kuu nchini Uingereza katika mwaka 2002 na 2004 kabla ya kufikia hatua ya fainali kwa mara nyingine ya kombe la UEFA hapo 2006 dhidi ya Barcelona FC katika jiji la Paris nchini Ufaransa pale Stade de France akiwa na wachezaji mahiri kabisa kama Thiery Henry,Robert Pires,Gilberto Silva,Fredrik Ljungberg,Ashley Cole,Jens Lehman na wengnineo,enzi izo Van Persie,Gael Clichy,Dennis Bergkamp,Jose Antonio Reyes,Plilippe Senderos,Flamini  wakisuburi benchi .
Katika kipindi hiki chote Arsenal ilikua ni timu yenye wachezaji mahiri na wenye kuimiri vishindo,kashkash na mikikimikiki ya ligi kuu na hata ile ya ligi bora kabisa duniani,ligi ya mabingwa katika nchi za Ulaya.
Miaka michache baadaya klabu hii hii chini ya kocha wake  huyuhuyu,dunia imeshuhudia madiliko hasi kwani klabu hii imegeuka kuwa mithiri ya kiwanda cha kuzalisha vipaji na kisha kuwauza katika vilabu vikubwa vyenye kutoa vitita vya pesa na zaidi,vilabu vyenye kiu na mataji.Hii imepelekea kumuangalia Wenger katika jicho jingine kabisa,hili ni jicho la ubahiri au kiutaalamu akiitwa mchumi na walio wengi,sababu za watu kuamua kumuita hivyo ni kutokana na yanayoendelea klabuni hapo,kuwauza wachezaji makini na wenye jeuri ya kuiletea klabu vikombe na kuacha kusajili wachezaji wenye hadhi ya kushindana na timu kubwa akisingizia katika miaka michache iliopita kuwa anafanya kukuza vipaji vitakavyoweza kuitetea klabu hio katika miaka ya usoni,lakini tunalo lishuhudia ni wachezaji kukua na wale walio bora zaidi kuuzwa katika vilabu vikubwa.Hii inatoa picha mbili,kiuchumi ni kweli klabu inanufaika kwa kupata faida kubwa kwani mishahara anayowalipa wachezaji walio wengi ni midogo na bado akiwauza wachezaji anawauza kwa pesa nyingi lakini katika upande wa pili wa shilingi anawaumiza mashabiki wa klabu hii kwani wanaishia kushuhudia timu nyingine zilizo makini zikibeba vikombe.
Soka la leo linahitaji Pesa kama kitu cha kwanza.Arsenal FC ni klabu yenye pesa lakini matumizi yake hayaonekani zaidi machoni pa wadau kama klabu nyingine kubwa zifanyavyo katika soka la leo.Katika miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia jeuri ya pesa katika kuleta mapinduzi,Manchester City FC wameweza kuleta mapinduzi katika ligi kuu nchini Uingereza na hata katika zile klabu nne bora, ‘’big four’’ kukitokea upinzani wa aina  yake,bado tumeweza kushuhudia huko nchini Ufaransa PSG pamoja na Monaco zinavyofanya mapinduzi,yote hii ikiwa ni jeuri ya pesa.
Machache ya kumalizia kuhusu klabu hii na hasa kupitia meneja wake,ni kutambua alama za nyakati  na kuwatendea haki mashabiki wake.Pesa ndio silaa pekee katika kupata wachezaji makini na mwisho wa siku kubeba vikombe.

mwandishi wa makala hii na msanifu wa goloso kwa habari za kimataifa

Wednesday, 5 March 2014

PICHA YA SIKU


MATOKEO YOTE INTERNATIONAL FRIENDLY MECHI


FT Japan 4 - 2 New Zealand
FT India 2 - 2 Bangladesh
FT Malawi 1 - 4 Zimbabwe
FT Burundi 1 - 1 Rwanda...
FT Georgia 2 - 0 Liechtenstein
FT Iran 1 - 2 Guinea
FT Kosovo 0 - 0 Haiti
FT Russia 2 - 0 Armenia
FT Zambia 2 - 1 Uganda
FT Azerbaijan 1 - 0 Philippines
FT Lithuania 1 - 1 Kazakhstan
FT Bulgaria 2 - 1 Belarus
FT Burkina Faso 1 - 1 Comoros
FT Mozambique 1 - 1 Angola
FT Albania 2 - 0 Malta
FT Algeria 2 - 0 Slovenia
FT Greece 0 - 2 South Korea
FT Hungary 1 - 2 Finland
FT Mauritania 1 - 1 Niger
FT Montenegro 1 - 0 Ghana
FT South Africa 0 - 5 Brazil
Imeahirishwa. Sudan ? - ? Kenya
FT Czech Republic 2 - 2 Norway
FT Bosnia-Herzegovina 0 - 2 Egypt
FT Andorra 0 - 3 Moldova
FT Botswana 3 - 0 South Sudan
FT Colombia 1 - 1 Tunisia
FT Cyprus 0 - 0 N.Ireland
FT FYR Macedonia 2 - 1 Latvia
FT Senegal 1 - 1 Mali
FT Luxembourg 0 - 0 Cape Verde
FT Namibia 1 - 1 TANZANIA
FT Turkey 2 - 1 Sweden
FT Morocco 1 - 1 Gabon
FT Romania 0 - 0 Argentina
FT Ukraine 2 - 0 USA
FT Gibraltar 0 - 2 Estonia


Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kimekwenda sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya timu ya taifa Namibia, katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki unaotambuliwa na Fifa uliochezwa Jumatano usiku kwenye uwanja wa Sam Nujoma nchini Namibia.

Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika,timu hizo zilikuwa bado hazijafungana,na kocha Salum Madadi akafanya mabadiliko katika kipindi cha pili kwa kuwatoa Erasto Nyoni, Ramadhani Singano na juma Luizio, na nafasi zao kuchukuliwa na Michael Aidan, Atanas Mdam na Hamis Mcha.

Stars ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 86 kwa mkwaju wa kona  uliopigwa na Hamisi Mcha aliyetokea benchi na mpira kuingia moja kwa moja bila kuguswa.

Namibia walisawazisha bao hilo katika dakika ya 95 lililofungwa na Nekundi Haleluya Panduleni, baada ya kupigwa mpira wa adhabu.
 
Lakini katika hali ya kushangaza waamuzi toka nchini Zambia na msimamizi wa mechi toka nchini Afrika Kusini waliopangiwa kuchezesha mchezo huo hawakutokea,na badala yake shirikisho la soka Namibia NFA,wakaamuru mchezo huo uchezeshwe na waamuzi wa Namibia kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Mwalimu Salum Madadi alisema licha ya kuwakosa wachezaji wengi nyota, kikosi hiki kilipigana hadi dakika ya mwisho na ameridhishwa na matokeo yaliyopatikana.

Wachezaji walioshindwa kujiunga na kikosi cha Stars ni Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Mwinyi Kazimoto ambao hawakuruhusiwa na vilabu vyao kutokana na kukosekana na usafiri wa kuwarudisha vilabuni kwa muda unaotakiwa.

Wengine walioshindwa kufika ni Edward Charles na Hassan Masapili ambao hati zao za kusafiri hazikuwa zimekamilika wachezaji wa Yanga ambao wako cairo hawakuweza kujiunga na taifa kwa sababu ya mechi yao ya marudiano na al alhaly ya misri.

Matokeo haya huenda yakaiweka Stars kwenye nafasi nzuri ya viwango vya Fifa kwa kupata sare ugenini.