GOLOSO LA SOKA
Na Kway Yudathadei
Arsenal ni kati ya
klabu kubwa,maarufu,yenye uwezo kifedha
na zaidi yenye mashabiki lukuki katika kona mbali za sayari hii ya Dunia
nisijue zaidi hata nje ya mipaka ya dunia hii.Ni mengi yanaweza kuzungumziwa
kuhusu klabu hii lakini nitapenda kuyaweka hadharani katika dawati hili la soka
machache tu ninayohisi yataweza kuwagusa
wadau .
Klabu hii ni ya mpira
wa miguu(soka) yenye maskani yake katika
eneo liitwalo Holloway huko kusini mwa Jiji la London na ilianzishwa
mnamo mwaka 1886 japokua mafanikio yake yalianza kuonekana zaidi katika miaka
ya 1930.
Katika kuitazama
Arsenal ya kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka
2014 yako machache ya kusemea.Klabu hii imeweza kupata mataji mawili tu ya ligi
kuu ya nchini Uingereza na mataji hayo yalipatikana katika misimu ya 2001/2002
na 2003/2004.Hizi ni enzi ambazo Arsenal FC waliweza kuijulisha dunia ni kwa
jinsi gani wanaweza kulitandaza soka sio tu kuishia kupiga pasi zenye macho ila
hata kupachika mabao na kuzuia wapinzani wao kupitia mabeki mahiri kabisa
waliokuwa nao enzi hizo.
Arsene Wenger ni kocha
aliye kabidhiwa majukumu ya kuinoa timu hio katika mwaka 1996 na alidhihirisha
ubora wake kwani ukiachana na kuchukua
kombe la ligi kuu miaka miwili baada ya yeye kuanza kuinoa timu hio na hata
kufanya usajili wenye manufaa kwa kuwanunua wachezaji makini kama Patrick
Vieira,Emmanuel Petit,Marc Overmars,Nicolas Anelka na wengineo wengi,mwaka 2000 aliiwezesha timu
hio kufika katika hatua ya Fainali ya kombe la mabingwabarani Ulaya,aliendeleza
ubabe kwa kuchukua kombe la ligi kuu nchini Uingereza katika mwaka 2002 na 2004
kabla ya kufikia hatua ya fainali kwa mara nyingine ya kombe la UEFA hapo 2006
dhidi ya Barcelona FC katika jiji la Paris nchini Ufaransa pale Stade de France
akiwa na wachezaji mahiri kabisa kama Thiery Henry,Robert Pires,Gilberto Silva,Fredrik
Ljungberg,Ashley Cole,Jens Lehman na wengnineo,enzi izo Van Persie,Gael
Clichy,Dennis Bergkamp,Jose Antonio Reyes,Plilippe Senderos,Flamini wakisuburi benchi .
Katika kipindi hiki chote
Arsenal ilikua ni timu yenye wachezaji mahiri na wenye kuimiri
vishindo,kashkash na mikikimikiki ya ligi kuu na hata ile ya ligi bora kabisa
duniani,ligi ya mabingwa katika nchi za Ulaya.
Miaka michache baadaya
klabu hii hii chini ya kocha wake
huyuhuyu,dunia imeshuhudia madiliko hasi kwani klabu hii imegeuka kuwa
mithiri ya kiwanda cha kuzalisha vipaji na kisha kuwauza katika vilabu vikubwa
vyenye kutoa vitita vya pesa na zaidi,vilabu vyenye kiu na mataji.Hii
imepelekea kumuangalia Wenger katika jicho jingine kabisa,hili ni jicho la
ubahiri au kiutaalamu akiitwa mchumi na walio wengi,sababu za watu kuamua
kumuita hivyo ni kutokana na yanayoendelea klabuni hapo,kuwauza wachezaji
makini na wenye jeuri ya kuiletea klabu vikombe na kuacha kusajili wachezaji
wenye hadhi ya kushindana na timu kubwa akisingizia katika miaka michache iliopita
kuwa anafanya kukuza vipaji vitakavyoweza kuitetea klabu hio katika miaka ya
usoni,lakini tunalo lishuhudia ni wachezaji kukua na wale walio bora zaidi
kuuzwa katika vilabu vikubwa.Hii inatoa picha mbili,kiuchumi ni kweli klabu
inanufaika kwa kupata faida kubwa kwani mishahara anayowalipa wachezaji walio
wengi ni midogo na bado akiwauza wachezaji anawauza kwa pesa nyingi lakini
katika upande wa pili wa shilingi anawaumiza mashabiki wa klabu hii kwani
wanaishia kushuhudia timu nyingine zilizo makini zikibeba vikombe.
Soka la leo linahitaji
Pesa kama kitu cha kwanza.Arsenal FC ni klabu yenye pesa lakini matumizi yake
hayaonekani zaidi machoni pa wadau kama klabu nyingine kubwa zifanyavyo katika
soka la leo.Katika miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia jeuri ya pesa katika
kuleta mapinduzi,Manchester City FC wameweza kuleta mapinduzi katika ligi kuu
nchini Uingereza na hata katika zile klabu nne bora, ‘’big four’’ kukitokea
upinzani wa aina yake,bado tumeweza
kushuhudia huko nchini Ufaransa PSG pamoja na Monaco zinavyofanya
mapinduzi,yote hii ikiwa ni jeuri ya pesa.
Machache ya kumalizia
kuhusu klabu hii na hasa kupitia meneja wake,ni kutambua alama za nyakati na kuwatendea haki mashabiki wake.Pesa ndio
silaa pekee katika kupata wachezaji makini na mwisho wa siku kubeba vikombe.
mwandishi wa makala hii na msanifu wa goloso kwa habari za kimataifa
0 comments:
Post a Comment