Baada
ya ukimya na utata, sasa imetangazwa kuwa mechi kati ya mabingwa
Afrika, Al Ahly na wale wa Tanzania Bara, Yanga itapigwa kwenye Uwanja
wa Max mjini Alexandria.
Mji
huo uko kwenye pwani ya bahari ya Mediterranean, kilomita zaidi ya 200
kutoka katika jiji hili la Cairo, mwendo wa zaidi ya masaa mawili.
Awali
ilikuwa siri, lakini leo mchana kiongozi wa umoja wa klabu za Misri,
Tharwat Swelam ameviambia vyombo vya habari mechi hiyo itapigwa bila ya
mashabiki.
“Lakini muda utakuwa ni saa moja usiku (saa mbili Bongo) kama ilivyopangwa awali, pia hatutaruhusu mashabiki,” alisema.
Kutokana na uamuzi huo, Yanga sasa inalazimika kusafiri tena kwenda Alexandria na bado uongozi wake haujatoa msimamo wake.
Awali
uongozi wa Yanga ulisema kama mechi itachezwa Alexandria basi lazima
wapewe ndege,
“Mechi
ikibadilishwa baada ya siku tatu kabla ya siku iliyopangwa hakuna
tatizo kwa sheria za Caf na pake Alexandiria si mbali,” alisema Mohamed
Mowad ambaye ni mkurugenzi wa masuala ya habari.
Suala
hilo lilikuwa na utata mkubwa, lakini mwisho limefikia hapo na
ainaonekana Al Ahly wana hofu ya kufanyiwa fujo na mashabiki wao iwapo
watapoteza mchezo huo.
Lakini Watanzania wanaoishi hapa wanasema hizo ni mbinu za kuwavuruga Yanga ili wazidi kuchanganyikiwa.
Baadaye jioni, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema amepata taarifa hizo na tayari analifanyia kazi.
"Kweli tumepata taarifa hizo na tayari tumeanza kulifanyia kazi suala hilo," alisema Sanga.
0 comments:
Post a Comment