GOLOSO LA SOKA
Na yudathadei kway
0768-154424
Nianze kwa kuwasabahi, kila mdau
kwa nafasi yake.Ni kwa mara nyingine tunakutana hapa kijiweni katika dawati
hili la michezo na burudani tukijaribu kuumiza bongo zetu.Basi leo ninakuja na
mada ya moto kati ya mada za moto nje ya
mipaka ya nchi yetu hususani katika Bara la Ulaya,bara linaloonekana kua na
mvuto zaidi katika tasnia hii ya soka na zaidi tukijikita katika viunga vya
jiji la Manchester katika klabu kongwe ya Manchester United FC.
Klabu hii ilianzishwa hapo mwaka
1878 na kuitwa Newton Heath LYR Football Club na mnamo mwaka 1902 jina
likabadilishwa na kuwa Manchester United.Klabu hii imekua na mafanikio makubwa
chini ya makocha mbalimbali wakiwa wameharibu rekodi zilizowekwa na makocha
wengine lakini pia wakiweka na wengine kuvunja rekodi katika klabu hii kongwe.
Leo hii ni katika kumuangazia
kocha wa sasa David Moyes aliye rithi mkoba ya babu Sir Alex Ferguson.Moyes
amekua na wakati mgumu sana kiujumla katika klabu hii ya Greater Manchester na
hii imechochewa na sababu mbalimbali kulingana na mitazamo na maono ya wadau
tofautitofauti.Katika kupunguza ukosefu wa vithibitisho,basi tujaribu
kuzitazama rekodi mbalimbali alizoweka kwa kuharibu za zamani lakini pia
tuziangalie zilezilizovunjwa na meneja huyu
Rekodi ya kwanza kuwekwa na kocha
huyu ni ile ya kuwa kocha wa kwanza kabisa kuanza majukumu yake na kubeba
kikombe,Ilikua mnamo tarehe 11 mwezi wa nane ambapo magoli mawili ya mpachika
magoli mahiri Robin Van Persie alipowatungua Wigan magoli mawili bila na
kuiwezesha klabu yake kutwaa ngao ya
hisani.
Rekodi nyingne ni ile iliyowekwa
na klabu hii chini ya kocha wake huyu ya kushinda mechi yake ya kwanza ya ligi
kuu nchini uingereza tokea mwaka 1977 timu hii ilipokuwa chini ya kocha Dave
Sexton. Rekodi hii iliwekwa katika dimba la Liberty Stadium likitazamwa na
mashabiki wapatao 20,733 kwa Manchester United kuichabanga Swansea
magoli manne kwa moja.
Lakini pia kocha huyu ameiwezesha
klabu hii kupata ushindi mnono ugenini katika makombe yanayo
shirikisha vilabu vya Ulaya tokea hapo mwaka 1957 ambapo kocha Busly Babes alipoiadhibu
Ireland’s Shamrock Rovers kwa magoli sita bila.Moyes amekuja kukumbushia hayo
kwa kuiongoza timu yake kuilabua klabu ya nchini ujerumani,Bayer Leverkusen kwa
magoli matano bila hapo tarehe 27 ya mwezi wa kumi na moja
Kocha huyu pia ameweza kuvunja
rekodi zilizowekwa na makochawengine katika klabu hii kwa kumsainisha mkataba
mnono katika klabu hio na hata katika klabu nyingine zote katika ligi kuu ya
Uingereza mchezaji wake Wayne Rooney.Mchezaji huyo raia wa uingereza amesaini
mkataba wa kumfunga klabuni hapo kwa miaka mitano na nusu akiwa analipwa paundi
300000 kwa wiki na katika kipindi chote cha mkataba kusadikika kupata paundi
milioni 85.
Rekodi nyingine aliyowekwa ni ile
ya kumsajili kiungo mshambuliaji Juan Mata kutoka katika klabu ya Chelsea FC
kwa kitita cha paundi milioni 37.1 na kuvunja rekodi ya uhamisho klabuni hapo
mnamo mwaka 2008 kwa Sir Alex kumsajili kutoka Totenham mchezaji Dimitar
Berbatov kwa kitita cha paundi milioni 30.75.Ikiunganishwa na uhamisho wa
kiungo mkabaji Marouane Fellaini kutoka Everton katika majira ya joto
ulioighaimu klabu ya Man U paundi milioni 27.5,David Moyes anaweka rekodi nyingine
kwa kutumia kiasi kikubwa kabisa cha pesa katika msimu mmoja kipatacho paundi
milioni 64.6.
Kocha huyu pia ameweza kuweka
rekodi mbovu klabuni hapo katika msimu wake wa kwanza katika kuinoa klabu hii
na kua katika ya vigezo hasi kwa wadau wa soka mpaka kuanza kuutilia mashaka
ufanisi wake wa kazi kulinganisha na makocha wengine,rekodi hizi ziko hapa
chini katika mapana yake
Mpaka sasaivi klabu hii kongwe
imefungwa mechi zipatazo nane katika ligi kuu na bado ikiwa na kibarua kikubwa
katika mechi za usoni.Tukirejea karika historia ya klabu hii inaonekana katika
misimu miwili,ya 2001-2002 na 2003-2004 klabu hii ilipoteza mechi tisa kila
msimu lakini bado ilimaliza ikiwa nafasi ya tatu katika kila msimu.Tusubiri
mpaka mwisho wa msimuilituone itakuaje.
Rekodi nyingine mbaya kwa kocha
huyu ni ile ya Manchester city FC kuiadhibu man U magoli manne kwa moja katika
dimba la Etihad.Kwa mara ya mwisho ilitokea katika dimba hilohilo mnamo mwaka
wa 1989 ambapo Man U waliadhibiwa vikali kwa magoli matano kwa moja.
Kuthibitisha ni jinsi gani mpaka
timu ndogo kimafanikio zinavojizolea sifa kutoka kwa mashabiki wao na hata
kuwapa mashabiki wa timu pinzani na man U kupata mwanya wa kuiogelea vibaya
timu hii,Klabu ya Stoke City,the potters imefanikiwa kuichachatya man U katika
msimu huu,mara yao ya mwisho ikiwa ni mwaka 1984.
Lakini pia Newcastle United
kupitia mshambuliaji wake Yohan Cabaye,imeweza kukata kiu yake ya miaka 41 bila
kuifunga Manchester united katika dimba la Old Trafford.Katika mechi zipatazo
32 man U wamekua wakiibuka washindi lakini Cabaye aliweza kuharibu rekodi hii
chini ya kocha David Moyes.
Katika michuano ya vilabu barani
ulaya,David Moyes amezidi kujiharibia sifa klabuni hapo kwa kipigo cha mbili
bila kutoka kwa klabu ya Olympiakos katika hatua ya 16 bora na hivyo kuwa klabu ya kwanza ya ugiriki kuifunga Man
U katika hatua hii.
Katika kuhitimisha,sitaki kutoa
tamko lolote kumhusu David Moyes kwani nahisi bado ni mapema sana kulingana na
uhalisia wa klabu ya Man U kwa makocha wake kihistoria.Lakusema hapa ni moja tu
kulingana na uhalisia wa soka,iwe timu ya klabu au timu ya taifa,’’Soka ni sawa
na mashua baharini,mawimbi yakitanda mashua hupata wakati mgumu katika safari
yake mithiri ya tumbo kuvurugika na mawimbi
yakitulia hali hua shwari’’.Tukutane kijiweni wakati mwingine wadau,Hili ndilo
dawati la soka bhana.
mwadishi wa makala hii ni msanifu wa habari za kimataifa wa goloso
0 comments:
Post a Comment