Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kimekwenda sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya timu ya taifa Namibia, katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki unaotambuliwa na Fifa uliochezwa Jumatano usiku kwenye uwanja wa Sam Nujoma nchini Namibia.
Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika,timu hizo zilikuwa bado hazijafungana,na kocha Salum Madadi akafanya mabadiliko katika kipindi cha pili kwa kuwatoa Erasto Nyoni, Ramadhani Singano na juma Luizio, na nafasi zao kuchukuliwa na Michael Aidan, Atanas Mdam na Hamis Mcha.
Namibia walisawazisha bao hilo katika dakika ya 95 lililofungwa na Nekundi Haleluya Panduleni, baada ya kupigwa mpira wa adhabu.
Lakini katika hali ya kushangaza waamuzi toka nchini Zambia na msimamizi wa mechi toka nchini Afrika Kusini waliopangiwa kuchezesha mchezo huo hawakutokea,na badala yake shirikisho la soka Namibia NFA,wakaamuru mchezo huo uchezeshwe na waamuzi wa Namibia kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Mwalimu Salum Madadi alisema licha ya kuwakosa wachezaji wengi nyota, kikosi hiki kilipigana hadi dakika ya mwisho na ameridhishwa na matokeo yaliyopatikana.
Wachezaji walioshindwa kujiunga na kikosi cha Stars ni Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Mwinyi Kazimoto ambao hawakuruhusiwa na vilabu vyao kutokana na kukosekana na usafiri wa kuwarudisha vilabuni kwa muda unaotakiwa.
Wengine walioshindwa kufika ni Edward Charles na Hassan Masapili ambao hati zao za kusafiri hazikuwa zimekamilika wachezaji wa Yanga ambao wako cairo hawakuweza kujiunga na taifa kwa sababu ya mechi yao ya marudiano na al alhaly ya misri.
Matokeo haya huenda yakaiweka Stars kwenye nafasi nzuri ya viwango vya Fifa kwa kupata sare ugenini.
0 comments:
Post a Comment