Pages

Saturday, 21 December 2013

SIMBA NDIO MTANI JEMBE WAIFUNGA YANGA TATU KWA MOJA

 Wachezaji wa Simba na baadhi ya viongozi wao wakipozi na kombe lao kwa furaha baada ya kukabidhiwa kombe hilo kwa kuifunga Yanga katika mchezo wa Nani Mtani Jembe, uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Simba wameibuka washindi kwa.kuichapa Yanga mabao 3-1, mabao ya Simba yalifungwa na Hamis Tambwe mawili na Awadhi Juma huku la kufutia machozi la Yanga likifungwa na Emmanuel Okwi.
 Meneja wa Yanga, Afidh Ally akipokea mfano wa hundi ya zaidi  sh. 98 milioni Kwa kuibuka washindi katika shindano la Nani Mtani Jembe kwa kupata kura nyingi katika unywaji wa bia ya Kilimanjaro.
Kiongozi wa Simba Hans Pope, akimpongeza Henry Joseph, baada ya mchezo huo. 

0 comments:

Post a Comment