LIWALO NA LIWE BRAZIL 2014
-Baada ya pilikapilika za
kumalizia kwa mechi za mtoano hatimaye liwalo na limekuwa mataifa 32 yamefuzu
kwenda kombe la dunia Brazil 2014 kwa bara la Africa wababe Ivory Coast,
Cameroon, Ghana, Nigeria na Algeria, wakati bara Asia ni Australia, Japan, Iran,
na Korea Kusini, huku bara lenye timu nyingi la ulaya mataifa ya Ubelgiji, Bosnia,
Italia, Urusi Ugiriki, England, Ujeruman, Uswisi, Ureno, Hispania, Ufaransa,
Croatia, na Uholanzi, Amerika ya kaskazini itakuwa inawakilishwa na mataifa ya
Costa Rica, Honduras, Marekani na Mexico wakati bara mwenyeji kutakuwa na
mataifa ya Argentina ya Messi, Colombia, Ecuador, Uruguay, Chile na mwenyeji Brazil
ya Neymar
Imekua ni njozi ya wachezaji wengi kucheza na zaidi kuonyesha
makali yao katika mitanange ya kombe la dunia, kwani hata mchezaji awe ana mafanikio makubwa kiasi gani katika klabu
aliopo hua wanahisi kukamilisha ndoto yao ya mafanikio katika michuano ya kombe
la dunia. Hayo yamethibitika hivi karibuni baada ya mchezaji alie katika
kiwango cha juu kabisa duniani na hata kuthibitisha makali yake kwa kuchukua
tuzo lukuki zikiwemo za mchezaji bora kabisa wa dunia, Leonel Messi aliekiri ya
kwamba furaha yake katika soka itakamilika tu endapo ataisaidia taifa lake
kuchukua kombe la dunia.
Wachezaji wanaorindima
katika kabumbu la vilabu huumia sana wanapokosa nafasi ya kucheza katika
michuano ya kombe la dunia hilo limeonekana kwa wachezaji wengi na mmoja wao ni
Zlatan aliepatwa na kiwewe kama sio gadhabu baada timu yake ya taifa kukosa
ticket ya kucheza kombe la dunia huko Brazil mwakani na kutamka ya kua, ’’michuano
hio haita pata mashiko au haita noga pasipo uwepo wangu’’. Jambo ambali sitaki
kuliamini sana.
Bado michuano ya kombe
la dunia hua ni nafasi tosha ya vilabu
kupata kujionea vipaji kutoka katika mataifa mbali mbali,mifano iko mizuri
lakini mfano uliobayana ni ule wa kinda katika enzi hizo Ronaldnho alieaminiwa
na kocha wake Luiz felipe scolari kwa kumfanya mbadala wa gwiji wa soka,Romalio
mbali ni vitisho na lawama za kutosha kutoka kwa wabrazil. Pia kombe la dunia
pale bondeni kwa mzeee Madiba liliibua vipaji vingi vingi kama akina Suarez kwa
Uruguay, Chicharito kwa Mexico, Ozil na Khedira kwa Ujerumani,
Na sasa ni wasaha
mwingine tena timu zikiwa zimeshapatikana za kwenda kuwakilisha mataifa na hata
mabara yao huko katika nchi maridadi kabisa kwa fukwe zenye kila aina ya nakshi
nakshi na warembo maridadi kabisa bila ya kusahau kua ndio aridhi inayoamika na
wengi kwa kua na vipaji vya kutosha vyenye ustadi wa hali ya juu na hata style
yao aina ya samba yenye kuleta msisimko wa ajabu kwa watazamaji pindi vijana
hawa wawapo katika pitch, hii ni Brazil ama kwa hakika.
Wako wachezaji wengi
ambao wanafanya makubwa katika tasnia ya soka kupitia vilabu vyao, Basi
michuano hio ijayo ndio itakua mzani tosha wa kutoa ukweli ni nani aliemzito zaidi
katika kabumbu. Tunasubili kuona makali ya akina Falcao na Colombia yao, Hazard
na Ubelgiji, Ronado na Ureno, Neymar na Brazil, Kagawa na Japani, Yaya na Ivory
Coast, Ribery na Ufaransa, Messi na Argentina,
Dzeko na Bosnia, Baloteli na Italy pamoja Rooney na England na wengine wengi
Hitimisho katika haya
yoooote ni jukumu letu kutayarisha akili,macho na mioyo, yote haya ni katika
kutoa tathmini makini juu ya mrindimo wa michuano kabambe kabisa ya kombe la
dunia.Nani atakae kua kinara katika kuthibitisha makali yake katika kulitetea
taifa lake kama wengi wao wanavo pigana kufa na kupona katika vilabu vyao. Na
mwisho wa siku tusubili tuone makundi
manane yatakuwaje nani nani watambana katika makundi, liwalo na liwe yaani
mtoto hatumwi sokoni pale Brazil.
by YOSSIMA SITTA (goloso 4real)
0 comments:
Post a Comment