Pages

Friday, 20 December 2013

SIASA INAHITAJI MBINU NA AKILI SIO ELIMU PEKEE

Baada ya kuibuka sekeseke tete ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) lililosababishwa na waliojiita "wapenda mabadiliko" moja ya hoja za wachangiaji kwenye mitandao ya kijamii ilikuwa kuhusu elimu "ndogo kutawala elimu kubwa"

Mjadala huu uliakisi waraka wa siri uliohaririwa na Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba kuhusu mkakati wao wa kusaka uongozi ndani ya chama kwa kumuweka mtu wao mwenye elimu ya "kueleweka"

J, elimu ya kueleweka ndani ya siasa ni ipi? Katika kupata mwanga kuhusu hoja hii, hebu tuangazie siasa za kimataifa.

Afrika Kusini inaweza kutoa funzo kubwa kuhusiana na hii dhana ya akili kubwa na ndogo.

Rais Nelson Mandela alipokuwa anastaafu alimuandaa msomi Thabo Mbeki kuwa rais wa chama cha African National Congress (ANC) na Rais Afrika Kusini.

Mbeki, msomi wa daraja la juu, mwenye shahada ya kwanza na ya uzamili katika uchumi aliyoipatia Uingereza kati ya mwaka 1962 na mwaka 1966 alipendelea siasa za uchumi wa soko wenye kuimarisha mitaji.

Alijihusisha zaidi na ukuaji wa uchumi wa nchi yake huku akisahau kuwa taifa lake lilikuwa linakabiliwa na uwiano mbaya wa ugawanaji wa rasilimali za nchi hasa ardhi.

Hakuonesha mikakati yoyote ya kuwainua watu wa chini yake ambao walipambana vikali kuondoa ubaguzi wa rangi ili wafaidi matunda ya nchi yao.

Ghafla Mbeki akaonekana mwenye elimu ndogo kisiasa. Vijana wakampa kisogo. Naibu wake Jacob Zuma, ambaye hakuwahi kuingia katika chumba kiitwacho darasa, na ambaye hata kusoma na kuandika alijifunza mitaani kiujanja ujanja, ghafla akawa na akili kubwa ndani ya siasa za ANC.

Uchaguzi ulipowadia, Zuma aliukwaa urais wa ANC, akambwaga Mbeki kwa kura nyingi, Mwenyekiti wa chama ndiye huteuliwa kuwania urais. Wote ni mashahidi kwa kile kilichotokea; Zuma ndiye Rais wa Afrika Kusini.

Na huko Marekani, katika uchaguzi wa mwaka 1980, gavana wa California Ronald Reagan ambaye aliukwaa urais wa nchi hiyo, alikuwa msanii wa maigizo kwenye redio na runinga. Reagan hakuwa msomi wa hali ya juu kwa kulinganisha na viwango vya Marekani. Alikuwa na shahada ya uchumi na sosholojia.

Alikubalika kwa jinsi alivyozisoma vyema siasa za Marekani. Kampeni yake iliegemea katika kujenga Marekani yenye kuogopwa. Pia alielezea nia yake ya kuheshimu uhuru wa raia.

Ingekuwa Afrika, Reagan angeweza kujiongezea muhula mwingine kwani alimaliza vipindi vyake viwili akiwa anapendwa sana.

Wakati wa kampeni yake ya muhula wa pili, mwaka 1984, mpinzani wake Walter Mondale na kambi yake, waliutumia umri mkubwa wa Reagan kama nguzo yao kuu ya kampeni.

Reagan aliipata hiyo hivyo katika moja wapo ya midahalo, alisema, "Katika kampeni zangu, sitatumia kigezo cha umri kumhujumu mgombea mwenzangu kwa kuhoji umri wake mdogo wenye uzoefu mdogo pia"

Kauli hii iliwasisimua wasikilizaji wake. Reagan alishinda kwa kishindo.

Katika siasa za Tanzania, wafanya siasa wenye akili kubwa wamefanikiwa kusoma akili na kujua hulka za Watanzania.

Hawafanikiwi kwa sababu ya shahada za uzamili au uzamivu bali kwa kuzipima akili za Watanzania wa kawaida, wakagundua uelewa wao, kisha wakachukua njia sahihi ya kushughulika nao.

Kwa mfano, kwa hulka ya Watanzania ya woga wa mapambano ya kudai haki zao, imekuwa rahisi kulainika kwa mahubiri yanayoonya "acha kupambana" na wenye madaraka au mahubiri yasemayo wapinzani wakishinda nchi itaingia vitani.

Hivi anayeshinda anaanzisha vita? Hiyo imetokea wapi?

Umesikia Chama Cha Mapinduzi (CCM) "wakijilaani" kuchukua ardhi ya watu wa Mbarali na kumpa mwekezaji feki ambaye halimi ila anawakodishia wananchi ardhi yao wenyewe. Je, kwa kujilaani, wenzetu hawa, wanakuwa wenye akili kubwa? Mbona hawakutangaza kulirudisha hilo shamba kwa wananchi?

Kuna wale watuhumiwa wa ufisadi ambao wamechukua staili ya mwizi anayekimbia na fuko la pesa-mwizi ambaye akiwa anakimbizwa huchukua kiasi cha pesa na kuanza kurusha kama chambo kwa wale wanaomfukuza.

Je, wataendelea kumfukuza au wataokota pesa na kumwacha mwizi atokomee? Je, hii haiwezi kuwa akili moja wapo? Si kila uchao tunasikia harambee kwenye makanisa na kwenye vikundi vya vijana na kina mama?

Wanaoendesha harambee hizi ni walewale watuhumiwa wa ufisadi. Tunafurahia fedha zao, lakini hatuwakamati!

Kwa wanachama wenzangu akina Dk. Kitila na Mwigamba ambao walitengeneza waraka wa kampeni wenye kuchafua wakuu waliopo, hawakuona hatari ya kudhalilisha chama?

Ikiwa daktari mwenye shahada ya uzamivu anakiri kuhusika kuutengeneza na kuuhariri waraka huo, je, hawa wasomi wa kiwango hicho walishindwa kuona hatari hiyo? Hiyo tuiiteje ni akili kubwa au ndogo?

Mandela aliwahi kusema kuwa "rafiki yako akianguka mpe mkono ili umnyanyue". Haya aliyasema alipokwenda Marekani mwaka 1998 kumpa pole Rais Bill Clinton alipokumbwa na kashfa ya mapenzi na mfanyakazi wa Ikulu Monica Lewinsky. Je, kwa nini Dk. Kitila na wenzake walikosa busara hii?

Mimi nikiwa mwanachama wa Chadema, bado nina imani kubwa na viongozi wakuu wa chama - kamanda Freeman Mbowe na mtendaji mkuu, Dk. Wilbrod Slaa - na ni ukweli usiopingika, Chadema imejengeka sana na kuwa tishio kwa CCM kipindi cha uongozi wao, na kwa hiyo bado wanahitajika sana katika chama.

Kamanda Mbowe ni mhamasishaji mzuri na bingwa wa siasa za wakati huu. Ni mbunifu pia. Hata vazi la Chama alilobuni ni hamasa tosha! Hii ndiyo akili inayohitajika.

Na Christopher Muleja ( 0784 397350)
MAWIO Alhamisi, Desemba 19 - 25, 2013 (Uk. 18)

0 comments:

Post a Comment