GOLOSO LA SPORT
NA YUDATHADEI KWAY
Ligi ya mabingwa ulaya
ndio inayosadikika kuwa ligi bora kabisa duniani inayotoa kila aina ya ladha ya
mpira huu gumzo duniani,mpira wa miguu.Ndio ligi inayowakutanisha ma supastaa
wa aina hii ya mchezo.
Katika msimu huu wa hii
ligi mengi yameshuhudiwa na wadau wa tasnia hii ya mchezo katika hatua ya
mwanzo kabisa ya michuano hii ambapo baadhi ya vilabu vikubwa kama Napoli, Olympic
Marseille, Juventus, FC Porto, Benifica,
Ajax vikisogezwa kando na hatua za juu za michuano hii lakini pia vilabu
vingine vikiingia katika hatua inayofuata.Draw imefanyika na hatimaye kila moja
wapo ya kilabu imeshafahamu itavaana na nani.
Hakika mengi
yamefikirika, mengi yamezungumzwa nabado yanazungumzwa juu ya matokeo ya hii draw.Sitataka kugusia juu ya kila klabu
na kitakaekutana naye bali lengo langu ni kujaribu kugusia vilabu vya EPL vinavyoteka na kukonga nyoyo za
watanzania walio wengi
Nikianza na Arsenal FC,
washika mtutu wa Jiji la London ktika viunga vya Highbury; hakika hii ni klabu
iliozoea hii ligi kupitia kocha wake Arsene Wenger. Katika msimu huu wa EPL
imeweza kuonyesha ni jinsi gani ilivyo makinika na hata kuongoza ligi kuu
yaUingereza mpaka hivi leo mengi yameongelewa kuhusu chachu walio nayo hivi
sasa na baadhi wamethubutu kutoa maoni yao kama vile,ujio wa kijana machachari
kabisa mwenye kujua kulitumia guu lake la kushoto vilivyo katika kupiga chenga
na kupenyeza ngome za timu mbalimbali lakini zaidi katika kupiga pasi za
mwisho,hapa ninamzungumzia mjerumani mwenye asili ya kituruki Mesut Ozil alie
tokea Real Madrid lakini wengine wanatoa
maoni yao na kudai ni kwa sababu ya kujiamini kwa Kocha wake mzee Wenger
hasahasa baada ya Babu Sir Alex Ferguson kustaafu na Wenger kubakia kama kocha
mkongwe aliedumu na klabu yake kwa mda mrefu inayo ambatana na kuchipukia kwa
safu ya kiungo yenye morali ya kutosha ya vijana Carzola,Wilshere, Ramsey
wakiongozwa na kamanda wao Mesut Ozil. Klabu hii imeweza kupenyeza hata katika
kundi lililosemekana ni la kifo katika hatua ya kwanza ya ligi ya mabingwa
ulaya lililokua na timu za Dortmund, Napoli, Marseille na Arsenal. Katika hatua
hii ya 16 bora wamekutanishwa na miamba ya soko na bingwa watetezi Bayern
Muchen, Vijana wanaopiga soka la kiufundi, soka lenye taaluma kiufundi katika
Nyanja ya pasi, kasi na nguvu.klabu yenye wachezaji machachari wenye uchu na
ushindi katika kila game wanayocheza, akina Frank Ribery, Robben, Muller, Gotze,
Larm na wengineo wengi. Mengi yanaongelewa lakini yote katika yote ni kusubiria
kitakachojiri.
Tukiwageukia Vijana
wengine wa Jiji la London, the blues
walio chini ya kocha maarufu, kocha mtabe, kocha mwenye kuthubutu
kujaribu, kocha jeuri Jose Mourinho. Ni kati ya timu zinazoogopeka katika michuano
hii kwani ina vijana wenye vipaji na wenye hamasa kubwa ya mataji inayochochewa
na kocha wao Mourho. Imefanikiwa pia kufikia hatua ya kumi na sita bora ambapo
imepangwa na Klabu yenye uwezo pia ya Galatasary kutokea Uturuki. Kukutana kwa
timu hizi kunazua hisia kali za kutamani kushuhudia tifu lake kwasababu chache
kama, Didier Drogba kijana alieifanyia makubwa klabu ya Chelsea akiwa chini ya
Mou na hata baada ya Mou kuondoka bado akaisaidia klabu yake kubeba ubingwa wa
UEFA mwaka 2012 na kuinyang’anya bayern muchen tonge mdomoni katika uwanja wake
wa nyumbani, lakini pia ni kukutana wakiwa na timu mbili tofauti kocha Mou na
Kijana fundi wa kiholanzi Sneijder waliokua wote katika klabu ya International
Milan na wakifanikiwa kuchukua kombe la mabingwa la Ulaya mwaka 2009 bila
kusahau hamu ya kuona maajabu ya kocha Mancini akiwa
na kikosi cha miamba hio ya Uturuki.Tungojee kwa hamu maajabu ya mitanange hio
ninayoiita shupavu kwani timu hizi zote zina aina flani inayofanana kimchezo
kwa kutumia nguvu.
Katika kuwaangalia Man
City FC kutokea katika mitaa ya jiji la Manchester, Hii ni klabu ilio na
wachezaji mafundi na wenye kila aina ya mbinu ya kuikabili timu yoyote ile
chini ya kocha wake Pellagrin. Katika hatua ya 16 bora wamepata kupangwa na
timu machachari kabisa katika kupiga pasi za kifundi na kumiliki mpira
watakavyo wao, hawa ni vijana wa Catalunya Barcelona FC. miamba hii miwili
inavuta hisia za wakereketwa wa kandanda kwani wote wawili wako katika hari
mahiri kabisa ya kuchukua mataji,wakiongozwa na makocha wenye hekima ya kisoka
na wenye kila sababu ya kushinda kila mechi inayokua mbele yao kwa maana ya kua
na zana zenye makali ya kutosha lakini chachu nyingine inaletwa na uwepo wa
kijana mwenye tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika Yaya Toure alietokea Barcelona
na kutua Man City na kuonyesha kiwango bora kabisa na hata kusababisha maswali
mengi kwa wadau wa soka, Je ni kweli Barca walimuuza kwa kua alikua ameshuka
kiwango? Je ni kweli Sergio anakiwango cha kuweza kuchochea kuuzwa kwa Yaya?
Yote haya yanaweza jibiwa vyema kabisa na matches watakazokutana. Hatatumwa
mtoto dukani hapo .
Mabingwa watetezi wa
EPL Manchester United nao wako katika hatua hii ya 16 bora. Ni klabu ambayo iko
katika hatua au kipindi ambacho waingereza wanakiita ‘’transitional period’’
wakimaanisha kipindi cha mpito. Hii inasababishwa na kusadikika kwa kupungua
kwa makali ya klabu hio baada ya kustaafu kwa kocha wake Sir Alex na mikoba
yake kukabidhiwa David Moyes ambae mpaka sasaivi hajaonyesha kile ambacho
mashabiki wa klabu hii wamekua wakikizoea kipindi kile akiwepo babu Ferguson. Kwa
sasa klabu hii inashikilia nafasi ya 8 katika EPL jambo ambalo halikua rahisi
kutokea kipindi cha Sir Alex katika kipindi hiki cha Christmass.Wadau wanadai
kocha huyu apewe muda kwani mafanikio kimpira sio jambo la upesi. Basi katika
hatua hii ya 16 bora wamekabidhiwa vijana wa kigiriki. Olympiacos wenye uzoefu
na michuano hii na wenye uwezo pia kimpira. yetu ni macho katika kutizama, akili
katika kutathmini na maskio katika kusikia yatakayosemwa baada ya matches
katika kulinganisha fikra na mitizamo.
Kushinda kwa timu
yoyote kimpira kunategemea vitu kadhaa vikiwemo, makocha wenye hekima kisoka, machezaji
wenye viwango bora kabisa wawapo katika pitch, kuridhishwa kwa makocha na
wachezaji kimaslahi (uongozi bora wa vilabu) na hamasa au amshaamsha ya
mashabiki. Timu zote zinazoingia katika
ligi hii ya mabingawa ulaya zinakua na vigezo vyote hivi kwamaana nyingine ni
kwamba,’’zote zinakila sababu ya kushinda,hakuna timu ya kubeza’’.Tusubiri
kwa hamu yatakayojiri.
0768-154424
|
0 comments:
Post a Comment