Mzunguko wa kwanza kwa
ligi kuu umeisha na sasa tunasubiri mzunguko wa pili, Mbichi na mbivu tumeziona
usajili mbovu tumeuona, timu bora tumeiona, timu yenye nidhamu nayo tumeiona, waliochemka
nao hao tumewaona, wanafiki nao tumewaona, wanasiasa nao tumewaona,
Mgeni karibu wenyeji
apone, kuna wageni wengi tuliwakaribisha kabla ya kuanza msimu wa ligi kuu ya
Vodacom; timu, makocha, na wachezaji , mojawapo ni timu za Mbeya City, Ashati
United, na Rhino, makocha kibadeni (simba), mayanja (kagera), nkoma (rhino) na
wachezaji wengi wengi karibu kila timu ilikuwa na mgeni, wageni wengine
wameanza kuaga na kurudi makwao na wengine wakifukuzwa na wenyeji.
Kwa leo tunamuangalia
mgeni wa Simba Abdalah Kibadeni ambaye aliingia kwa mbwembwe na kukalibishwa
kwa furaha na wenyeji wake na sasa wamemuchoka mgeni wao na kuwaambia watoto
hebu mwambieni yule mgeni arudi kwao akawasalie hata kidogo, ndio tabia ya Simba
akienda tu utasikia kuna mgeni mwigine mpya, so hawamuhitaji tena ndio mbinu wanayoitumia.
walioitumia kuwafuta kazi Cirkovic na Lewing sijui kwa sasa kibadeni itakuwaje
maana yeye ni Mtanzani
Hakuna kitu kinachouma
kama kufukuzwa kwa kocha, Bora umalize mkataba ili uondoke mwenyewe kuliko
kufukuzwa. Abdalah King Kibadeni “Mputa”, kuna dalili za sitafahamu ndani ya
kilabu yake ya Simba. Kutokana na tabia ya klabu ya Simba, hizi ni sababu nne
ambazo zinafanya mgeni Kibadeni kuchokwe na Simba Sport Club.
-Sababu ya kwanza;
kulalamika kupangiwa kikosi. Jaman mgeni
anajichagulia chakula kwa mwenyeji leo nataka wali nyama, kesho ugali samaki ni
mgeni gani huyu. Lini kocha wa timu ya Simba huwa hapangiwi kikosi? waaulize wakina
Phiri, Cirkovic, Basena na Lewing walikuwa wanalalama kupangiwa vikosi. Lakini
ndio tabia na utamaduni wa vilabu vyetu, viongozi wanapanga vikosi, ndio
wanajua kesho nani anaanza kikosi cha kwanza na nani anaanzia bechi bila kuangalia performance ya mazoezi ya
wachezaji. Kibadeni alikuwa akilalama
kupangiwa baadhi ya wachezaji kwa matakwa ya viongozi kama Hamud kwenye mechi
ya Simba na Yanga, Mimi najiuliza kwa nini Kibadeni asigome kumpanga Hamud
mpaka matokeo yakawa mabaya ndio akaanza kulalama?
-Wachezaji ni sababu ya
pili ambayo itafanya Kocha kibadeni wamuchoke wenyeji wake. Muundo wa sasa wa Simba
kama mchezaji akicheza chini ya kiwango
au atofautiane na kocha au viongozi ni lazima ashushwe timu ya wadogo ili kurudisha kiwango. Sioni mantiki
ya Kibadeni na benchi lake la ufundi kufanya hivyo kwani anatengeneza bifu yeye
pamoja na wachezaji wake anaowarudisha kikosi cha pili kunoa makali. Hata kesho
Chanongo, Humud, na Ramadhani Chombo Redondo wakirudishwa kikosi cha wakubwa
hawatakuwa na morali kama ya kwanza kwenye kikosi, maana watakuwa wameathirika
kisaikolojia. Ona kama Henry Joseph walivyomurudisha timu ya wakubwa na mechi
ya mwisho dhidi ya Ashati alicheza lakini si Henry yule wa kipindi kile bado
hajarudishwa kikosi cha watoto.
-Sababu ya tatu ambayo
itafanya mgeni Kibadeni apewe likizo ya malipo ni matokeo. Simba ilianza vizuri
sana mwanzo wa ligi kwa kuongoza ligi, ila kuanzia kwenye mechi ya Yanga mambo yakaanza
kwenda mrama baada ya kutoa sare na Yanga Sport Club. Wakaenda Tanga tena nako
wakambulia suluhu pale Mkwakwani wakarudi tena Dar wakapata kipigo cha kwanza
toka kwa Wanalamba lamba Azam, wakazid
kuvurungwa zaidi na zaidi, wakaingia kucheza tena na Kagera wakaambulia tena
pointi moja. Katika mechi nne wameambulia pointi tatu na kupoteza pointi12 kabisa.
Kabla ya mechi ya mwisho kupata pointi tatu. Haya ni matokeo mabaya kutokea kwa
Simba msimu huu. Kibadeni watampa likizo maana Simba huwa wanawapa likizo makocha
wao hata anaongoza ligi. Basena aliongoza ligi ila walimpa likizo ya moja kwa
moja baada ya kufungwa na Yanga, Lewing naye hivyo hivyo, Cirkovic naye
walimuacha mzunguko wa kwanza na kumuajiri Lewing, sasa imefika zamu ya Kibadeni.
-Benchi la ufundi ni
sababu mojawapo ambayo inafanya Kibadeni achokwe Simba. Umeliona benchi la simba chini ya kocha
mkuu Kibadeni, msaidizi Julio na meneja Nicco Nyangawa wameshidwa kuimeneji
timu kabisa. Kila mtu ana maoni yake ndani ya kilabu. Kibadeni ni kocha mkuu
lakini naona kama anamuogopa Julio na kumuachia majukumu mengi ndani ya Simba.
Julio ndio anafanya kila kitu Simba, Mabadiliko ya wachezaji ndio amekuwa mtoa
ushauri kwa kocha, ndio muhamasishaji wa timu. Ni lini kocha msaidizi ndo
anakuwa na jukumu la kutoa maelekezo kwa wachezaji? umeona ulaya; sijawahi
kuwaona akina Mourinho, Moyes, na Anceloti
wakikaa kwenye bechi wasaidizi wao ndio wanasimama kutoa maelezo kwa
wachezaji labda kama kocha hayupo kwenye bechi ila kwa Simba hata Kibadeni yuko
kwenye benchi hukaa tu na Jamhuli Kiwelu Julio akitoa maelekezo.
0 comments:
Post a Comment