Pages

Tuesday, 31 December 2013

*KWAHERI 2013 KARIBU MWAKA MPYA 2014, HAPPY NEW YEAR WADAU WOTE WA GOLOSO

MECHI ZA KESHOOO. EPL

KESHO
- Januari 1, 2014.

15:45 Swansea City vs Manchester City

18:00 Arsenal vs Cardiff City ...

18:00 Crystal Palace vs Norwich City


18:00 Fulham vs West Ham United


18:00 Liverpool vs Hull City


18:00 Southampton vs Chelsea


18:00 Stoke City vs Everton


18:00 Sunderland vs Aston Villa


18:00 West Bromwich Albion vs Newcastle United


20:30 Manchester United vs Tottenham Hotspur

BAADHI YA VIWANJA MASHUHURI DUNIANI NA UWEZO WAKE



UINGEREZA
Old Trafford | Manchester United |
Ulifunguliwa | 1910...
Uwezo | Siti 75,811

Emirates Stadium | Arsenal FC |
Ulifugnuliwa | 2006
Uwezo | Siti 60,361

Anfield | Liverpool FC |
Ulifunguliwa | 1884
Uwezo | Siti 45,522

Stamford Bridge | Chelsea FC |
Ulifunguliwa mwaka | 1877
Uwezo | Siti 41,837

UJERUMANI
Allianz Arena | Bayern München & 1860 München
Ulifunguliwa | 2005
Uwezo | Siti 71,000

Signal Iduna Park | Borussia Dortmund
Ulifunguliwa | 1974
Uwezo | Siti 80,720 (25,000 wakisimama)

SPAIN
Camp Nou | FC Barcelona |
Ulifunguliwa | 1957
Uwezo | Siti 99,354

Estadio Santiago Bernabéu | Real Madrid CF |
Ulifunguliwa | 1947
Uwezo | Siti 85,454

ITALIA
San Siro | AC Milan na FC Inter |
Ulifunguliwa | 1926
Uwezo | Siti 80,018

Juventus Stadium | Juventus FC |
Ulifunguliwa | 2011
Uwezo | Siti 41,000

KLABU ZENYE MASHABIKI WENGI ZAIDI DUNIANI !



10. Juventus Ina Mashabiki Milioni 20

9. Bayern Munich Ina Mashabiki Milioni 24...

8. Inter Milan Ina Mashabiki Milioni 49

7. Liverpool Ina Mashabiki Milioni 71

6. AC Milan Ina Mashabiki Milioni 99

5. Arsenal Ina Mashabiki Milioni113

4. Chelsea Ina Mashabiki Milioni 135

3. Real Madrid Ina Mashabiki Milioni 174

2. Barcelona Ina Mashabiki Milioni 270

1. Manchester United Ina Mashabiki Milioni 354

Chanzo: Forbes football

Sunday, 29 December 2013

UNAIPATA HII MAN U

Name: Manchester United
Surname: Champion
Nickname: Red Devils
Age: 134 years
Birthday: 1878...
Hobbies: Victories
Location: Old Trafford
Titles: Unlimited
Colours: Red and white
LIKE: Trophies
Food: We eat all teams
Love: Red Devils
Wishes: All realized
Want to Say: Glory Glory Man United
Dreams: Reality (Other teams dreams not us )
Favorite saying: We always win!
House: You can find us at the Palace of Cups!
Happiness: When city,chelsea,li verpool lose.
products: Producer of goals
Tradition: Just stars and talents
History: Always legend

PICHA YA SIKU


Saturday, 28 December 2013

ASHANTI UNITED VS JKT RUVU KUJARIBU MATUMIZI YA TIKETI ZA ELEKTRONIKI JANUARY MOSI, CHAMAZI

Timu za Ligi Kuu za Ashanti United na JKT Ruvu Stars zinapambana Januari Mosi mwakani kati moja ya mechi za kujaribu matumizi ya tiketi za elektroniki kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Viingilio katika mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni sh. 1,000 na sh. 2,000 ambapo tiketi zinapatikana kupitia M-Pesa na mawakala wa CRDB Fahari Huduma. Tiketi zitaendelea kuuzwa hadi kipindi cha kwanza cha mechi hiyo kitakapomalizika.
Mawakala 18 wa Fahari Huduma wanaouza tiketi hizo ni ABC Computer- Mtaa wa Samora, Abraham Anangisye Mwampetele- Maji Matitu, Apex Security Services- Mtaa wa Mibega, Kinyerezi, Athuman Fakhi Adam- Kongowe Mbagala, Fedha Investment Limited- Pamba Road na Fuya Godwin Kimbita- Tegeta Block.
Ghomme Health & Education Limited-Bahari Beach, Herman Arbogast Tarimo- Kigamboni, K- Finance Limited- Shekilango, Sinza, Koli Finance Limited- Mtaa wa Samora, LB Pharmacy- Mtoni Kijichi, Lista Phares Barnabas- Tabata Segerea na Maly Investment Company Limited- Mtaa wa Sikukuu, Kariakoo.
Wengine ni Micu Enterprises- Mtaa wa Congo, Kariakoo, S&D Collection Company Limited- Mikocheni, Shoppers Plaza, Therry Investment Limited- Tegeta Kibaoni, TSHS Distributors Limited- Mtoni kwa Aziz Ali na Wemerick Independent Vehicle- Mtaa wa Boko.
Pia mshabiki anaweza kununua tiketi kwa njia ya simu- mtandao wa Vodacom kwa kupiga *150*03*02# ambapo atapata namba atakayoitumia kufanya malipo kupitia MPESA. Katika MPESA namba ya malipo kwa TFF ambayo ndiyo mshabiki ataitumia kufanya malipo ya tiketi (business number) ni 888800. Vilevile mteja wa CRDB aliye katika mtandao anaweza kufanya malipo kupitia CRDB simbanking.
Baada ya kufanya maombi kupitia njia yoyote ya hizo tatu; MPESA, Fahari Huduma na CRDB simbanking, mshabiki atapata namba ambayo ataitumia ku-print tiketi yake kupitia mashine maalumu za kuchapia Tiketi ya TFF zilizo katika ATM za CRDB kwenye maeneo yafuatayo;
Benki ya CRDB tawi la Azikiwe, tawi la Holland House ambapo kuna mashine mbili, tawi la Vijana, tawi la Kariakoo, ATM ya Mtaa wa Shaurimoyo ambapo kuna mashine mbili na ATM ya CRDB iliyoko kituo cha mafuta cha Kobil Sabasaba, Mtoni kwa Aziz Ali.

UTABILI WA MWANAGOLOSO KUHUSU MSIMAMO WA EPL MWISHO WA LIGI UTAKUWA HIVI


MECHI ZA EPL WEEKEND HII

LEO - Jumamosi 28 December 2013

15:45 West Ham United vs West Bromwich Albion

18:00 Aston Villa vs Swansea City...

18:00 Hull City vs Fulham


18:00 Manchester City vs Crystal Palace


18:00 Norwich City vs Manchester United 


20:30 Cardiff City vs Sunderland

KESHO - Jumapili 29 December 2013


16:30 Everton vs Southampton


16:30 Newcastle United vs Arsenal


19:00 Chelsea vs Liverpool 


19:00 Tottenham Hotspur vs Stoke City

KOMBE LA MAPINDUZI: KOCHA WA ITALIA PRANDELLI MGENI RASMI SIMBA VS AFC LEOPARDS



MAANDALIZI ya kombe la Mapinduzi linalotarajia kuanza kutimua vumbi januari mosi mwakani yanakwenda vizuri na timu zote zilizothibitisha kushiriki zinatarajia kuwasili desemba 31 mwaka huu.

Msemaji wa kamati ya mashindano , Farouk Karim amesema kuwa timu za Tusker fc, AFC Leopard za Kenya, KCC, URA za Uganda , Simba sc, Yanga, Azam fc na Mbeya City za Tanzania bara tayari zimeshathibitisha kushiriki na kamati ya maandalizi imeshakamilisha  taratibu za kuzipokea.

SIMBA imepangwa kufungua pazia la michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kucheza na AFC Leopards ya Kenya Januari Mosi wakati Yanga wakishuka dimbani siku inayofuata kuikabili Tusker FC.

Karim amesema mgeni rasmi katika mechi ya ufunguzi itakayopigwa januari mosi majira ya saa mbili usiku katika uwanja wa Aman kisiwani Unguja baina ya Simba sc dhidi ya AFC Leopard ya Kenya atakuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Italia,  Cesare Prandelli.

Pambano la Simba na Leopards litatanguliwa na mechi kati ya wenyeji KMKM na KCC ya Uganda litakalopigwa saa 10 jioni kwenye uwanja huohuo.

“Ninavyozungumza na wewe muda huu, Prandelli yupo hapa Zanzibar mapumzikoni na tayari amekubali kufungua michuano hii yenye maana kubwa katika miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar”. Alisema Karim.

Karim alisema katika michuano ya mwaka huu viwanja viwili vitatumika ambavyo ni Gombani kisiwani Pemba na Aman Kisiwani Unguja.

“Uwanja wa Gombani upo katika hali nzuri na unavyojua una nyasi za bandia. Uwanja wa Aman umefanyiwa ukarabati mkubwa na hivi sasa wataalamu kutoka China wapo hatua za mwisho kabisa kukamilisha shughuli yao”. Alisema Karim.
Mratibu huyo alitoa wito kwa wadau, wapenzi wa soka visiwani Zanzibar kujitokeza kwa wingi kwani kamati ya mashindano inategemea mapato ya milangoni kufanikisha mipango.

“Michuano hii inagharimu zaidi ya shilingi milioni 600, hatuna fedha hizo, tunategemea mapato ya milangoni, hivyo mashabiki kufika kwao  kwa wingi ndio mafanikio yetu”. Aliomba Karim.

Aidha ameziomba taasisi na makampuni ya bara na visiwani kujitokeza kufanya matangazo katika michuano hiyo ili angalau wapate pesa za kuendeshea michuano hiyo.

Michuano iliyopita, Azam fc walitwaa ubingwa, lakini mwaka huu kuna changamoto mpya hasa kutokana na uwepo wa timu za Dar Young Africans na Mbeya City ambazo hazikushiriki.

Mechi zote za hatua ya makundi na robo fainali zitafanyika kwenye viwanja wa Gombani Pemba na Aman Unguja, wakati nusu fainali na fainali zitapigwa kwenye Uwanja wa Amani.

Katika michuano iliyopita Simba waliishia nusu fainali baada ya kuondolewa na Azam FC kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya mechi kumalizika kwa sare ya 2-2 hata baada ya kuongezwa dakika 30.

Thursday, 26 December 2013

PICHA YA LEO


16 BORA YENYE MASHIKO UEFA

          
 GOLOSO LA SPORT
NA YUDATHADEI KWAY
Ligi ya mabingwa ulaya ndio inayosadikika kuwa ligi bora kabisa duniani inayotoa kila aina ya ladha ya mpira huu gumzo duniani,mpira wa miguu.Ndio ligi inayowakutanisha ma supastaa wa aina hii ya mchezo.
Katika msimu huu wa hii ligi mengi yameshuhudiwa na wadau wa tasnia hii ya mchezo katika hatua ya mwanzo kabisa ya michuano hii ambapo baadhi ya vilabu vikubwa kama Napoli, Olympic  Marseille, Juventus, FC Porto, Benifica, Ajax vikisogezwa kando na hatua za juu za michuano hii lakini pia vilabu vingine vikiingia katika hatua inayofuata.Draw imefanyika na hatimaye kila moja wapo ya kilabu imeshafahamu itavaana na nani.
Hakika mengi yamefikirika, mengi yamezungumzwa nabado yanazungumzwa juu ya matokeo ya  hii draw.Sitataka kugusia juu ya kila klabu na kitakaekutana naye bali lengo langu ni kujaribu kugusia vilabu  vya EPL vinavyoteka na kukonga nyoyo za watanzania walio wengi

Nikianza na Arsenal FC, washika mtutu wa Jiji la London ktika viunga vya Highbury; hakika hii ni klabu iliozoea hii ligi kupitia kocha wake Arsene Wenger. Katika msimu huu wa EPL imeweza kuonyesha ni jinsi gani ilivyo makinika na hata kuongoza ligi kuu yaUingereza mpaka hivi leo mengi yameongelewa kuhusu chachu walio nayo hivi sasa na baadhi wamethubutu kutoa maoni yao kama vile,ujio wa kijana machachari kabisa mwenye kujua kulitumia guu lake la kushoto vilivyo katika kupiga chenga na kupenyeza ngome za timu mbalimbali lakini zaidi katika kupiga pasi za mwisho,hapa ninamzungumzia mjerumani mwenye asili ya kituruki Mesut Ozil alie tokea Real Madrid lakini wengine  wanatoa maoni yao na kudai ni kwa sababu ya kujiamini kwa Kocha wake mzee Wenger hasahasa baada ya Babu Sir Alex Ferguson kustaafu na Wenger kubakia kama kocha mkongwe aliedumu na klabu yake kwa mda mrefu inayo ambatana na kuchipukia kwa safu ya kiungo yenye morali ya kutosha ya vijana Carzola,Wilshere, Ramsey wakiongozwa na kamanda wao Mesut Ozil. Klabu hii imeweza kupenyeza hata katika kundi lililosemekana ni la kifo katika hatua ya kwanza ya ligi ya mabingwa ulaya lililokua na timu za Dortmund, Napoli, Marseille na Arsenal. Katika hatua hii ya 16 bora wamekutanishwa na miamba ya soko na bingwa watetezi Bayern Muchen, Vijana wanaopiga soka la kiufundi, soka lenye taaluma kiufundi katika Nyanja ya pasi, kasi na nguvu.klabu yenye wachezaji machachari wenye uchu na ushindi katika kila game wanayocheza, akina Frank Ribery, Robben, Muller, Gotze, Larm na wengineo wengi. Mengi yanaongelewa lakini yote katika yote ni kusubiria kitakachojiri.


Tukiwageukia Vijana wengine wa Jiji la London, the blues  walio chini ya kocha maarufu, kocha mtabe, kocha mwenye kuthubutu kujaribu, kocha jeuri Jose Mourinho. Ni kati ya timu zinazoogopeka katika michuano hii kwani ina vijana wenye vipaji na wenye hamasa kubwa ya mataji inayochochewa na kocha wao Mourho. Imefanikiwa pia kufikia hatua ya kumi na sita bora ambapo imepangwa na Klabu yenye uwezo pia ya Galatasary kutokea Uturuki. Kukutana kwa timu hizi kunazua hisia kali za kutamani kushuhudia tifu lake kwasababu chache kama, Didier Drogba kijana alieifanyia makubwa klabu ya Chelsea akiwa chini ya Mou na hata baada ya Mou kuondoka bado akaisaidia klabu yake kubeba ubingwa wa UEFA mwaka 2012 na kuinyang’anya bayern muchen tonge mdomoni katika uwanja wake wa nyumbani, lakini pia ni kukutana wakiwa na timu mbili tofauti kocha Mou na Kijana fundi wa kiholanzi Sneijder waliokua wote katika klabu ya International Milan na wakifanikiwa kuchukua kombe la mabingwa la Ulaya mwaka 2009 bila kusahau hamu ya kuona maajabu ya kocha Mancini akiwa na kikosi cha miamba hio ya Uturuki.Tungojee kwa hamu maajabu ya mitanange hio ninayoiita shupavu kwani timu hizi zote zina aina flani inayofanana kimchezo kwa kutumia nguvu.

Katika kuwaangalia Man City FC kutokea katika mitaa ya jiji la Manchester, Hii ni klabu ilio na wachezaji mafundi na wenye kila aina ya mbinu ya kuikabili timu yoyote ile chini ya kocha wake Pellagrin. Katika hatua ya 16 bora wamepata kupangwa na timu machachari kabisa katika kupiga pasi za kifundi na kumiliki mpira watakavyo wao, hawa ni vijana wa Catalunya Barcelona FC. miamba hii miwili inavuta hisia za wakereketwa wa kandanda kwani wote wawili wako katika hari mahiri kabisa ya kuchukua mataji,wakiongozwa na makocha wenye hekima ya kisoka na wenye kila sababu ya kushinda kila mechi inayokua mbele yao kwa maana ya kua na zana zenye makali ya kutosha lakini chachu nyingine inaletwa na uwepo wa kijana mwenye tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika Yaya Toure alietokea Barcelona na kutua Man City na kuonyesha kiwango bora kabisa na hata kusababisha maswali mengi kwa wadau wa soka, Je ni kweli Barca walimuuza kwa kua alikua ameshuka kiwango? Je ni kweli Sergio anakiwango cha kuweza kuchochea kuuzwa kwa Yaya? Yote haya yanaweza jibiwa vyema kabisa na matches watakazokutana. Hatatumwa mtoto dukani hapo .

Mabingwa watetezi wa EPL Manchester United nao wako katika hatua hii ya 16 bora. Ni klabu ambayo iko katika hatua au kipindi ambacho waingereza wanakiita ‘’transitional period’’ wakimaanisha kipindi cha mpito. Hii inasababishwa na kusadikika kwa kupungua kwa makali ya klabu hio baada ya kustaafu kwa kocha wake Sir Alex na mikoba yake kukabidhiwa David Moyes ambae mpaka sasaivi hajaonyesha kile ambacho mashabiki wa klabu hii wamekua wakikizoea kipindi kile akiwepo babu Ferguson. Kwa sasa klabu hii inashikilia nafasi ya 8 katika EPL jambo ambalo halikua rahisi kutokea kipindi cha Sir Alex katika kipindi hiki cha Christmass.Wadau wanadai kocha huyu apewe muda kwani mafanikio kimpira sio jambo la upesi. Basi katika hatua hii ya 16 bora wamekabidhiwa vijana wa kigiriki. Olympiacos wenye uzoefu na michuano hii na wenye uwezo pia kimpira. yetu ni macho katika kutizama, akili katika kutathmini na maskio katika kusikia yatakayosemwa baada ya matches katika kulinganisha fikra na mitizamo.

Kushinda kwa timu yoyote kimpira kunategemea vitu kadhaa vikiwemo, makocha wenye hekima kisoka, machezaji wenye viwango bora kabisa wawapo katika pitch, kuridhishwa kwa makocha na wachezaji kimaslahi (uongozi bora wa vilabu) na hamasa au amshaamsha ya mashabiki.  Timu zote zinazoingia katika ligi hii ya mabingawa ulaya zinakua na vigezo vyote hivi kwamaana nyingine ni kwamba,’’zote zinakila sababu ya kushinda,hakuna timu ya kubeza’’.Tusubiri kwa hamu yatakayojiri.
0768-154424



Wednesday, 25 December 2013

WINGA MACHACHACHARI WA SIMBA NIDHAMU YAMPA MATUNDA



Ramadhani Singado 'Messi'

WINGA machachari wa Simba, Ramadhani Singano 'Messi' amesema pamoja na sifa na pongezi anazomwagiwa na mashabiki wa soka kutokana na kuongeza kiwango katika siku za karibuni, hatabweteka na kuvimba kichwa badala yake atazidi kujituma ili aweze kutimiza ndoto za kutamba kimataifa.

Aidha, mchezaji huyo aliyeng'ara kwenye pambano la Nani Mtani Jembe, na kusaidia Simba kuicharaza Yanga mabao 3-1, amewataka wachezaji wenzake kuzingatia mazoezi, kujituma, kujitunza na kuzingatia nidhamu ndani na nje ya uwanjani iwapo wanataka kufika mbali.

Akizungumza na GOLOSO katika mahojiano maalum juzi, Messi alisema anawashukuru wote wanaompongeza na kummwagia sifa kwa kung'ara pambano la Simba na Yanga, lakini alisema anachukua pongezi hizo kama changamoto kwake za kuongeza juhudi ili afike mbali zaidi.

Singano alisema hawezi kubweteka na kuvimba kichwa kwa pongezi hizo kwa kutambua kuwa mashabiki wa soka ni 'vigeugeu' wanaoweza kumgeuka wakati wowote atakapocheza chini ya kiwango, pia malengo yake ni kufika mbali zaidi na mahali alipo sasa.


"Nawashukuru wanaonimwagia pongezi, namshukuru Mungu kwa kunisaidia kuwa hivi nilivyo pamoja na makocha na wachezaji wenzangu, ila siwezi kubweteka badala yake nitajituma zaidi ili nifike mbali," alisema.

Singano alisema kiu yake siyo kucheza Simba tu na Taifa Stars, bali kucheza soka la kulipwa kitu anachoamini anaweza kutimiza kwani uwezo anao na hasa akimtegemea Mungu kumpa umri na siha njema.

Winga huyo, mmoja wa wachezaji wakiopandishwa kikosi cha kwanza cha Simba kutoka timu B, amekuwa gumzo ndani ya kikosi hicho na Taifa Stars kutokana na uwezo wake wa kupiga chenga, mbio na kufunga.
SOURCE: micharazomitupu.com

MECHI ZA LEO ALHAMISI EPL

15:45 Hull City vs Manchester United
18:00 Aston Villa vs Crystal Palace
18:00 Cardiff City vs Southampton
18:00 Chelsea vs Swansea City
18:00 Everton vs Sunderland
18:00 Newcastle United vs Stoke City
18:00 Norwich City vs Fulham
18:00 Tottenham Hotspur vs West Bromwich Albion
18:00 West Ham United vs Arsenal
20:30 Manchester City vs Liverpool

JAMES KISAKA AFARIKI DUNIA, MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI AMINA.


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa kocha wa makipa wa Simba, James Kisaka (57) kilichotokea leo asubuhi (Desemba 25 mwaka huu) katika Hospitali ya Burhani, Dar es Salaam.
Msiba huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu kwani Kisaka kabla ya kuwa kocha alikuwa mchezaji katika nafasi ya kipa. Mbali ya Simba, timu nyingine alizowahi kudakia ni Ndovu ya Arusha, Volcano ya Kenya na Small Simba ya Zanzibar.
Akiwa mwanafunzi Shule ya Sekondari Tambaza jijini Dar es Salaam aliwahi kuchezea timu za Oysterbay Stars, Eleven Stars ya Msasani, Sigara wakati ikicheza Ligi ya Temeke na Nyota Nyekundu kabla ya kutua Simba.
Pia alikuwemo kwenye timu ya Taifa ya vijana iliyokwenda Zimbabwe kwenye sherehe za uhuru wan chi hiyo mwaka 1980. Vilevile alikuwa mmoja wa wachezaji waliounda kombaini ya Tanzania ya UMISSETA akiwa na akina Said George, Nico Njohole, George Kulagwa na wengine. Hivyo mchango wake katika mchezo huu tutaukumbuka daima.
Kwa mujibu wa kaka wa marehemu, Benny Kisaka, James alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa miguu kufa ganzi na matatizo ya kutoona vizuri.
Msiba uko nyumbani kwake Mbezi Mwisho (Kwa Yusuf), na anatarajia kuzikwa nyumbani kwao Kijiji cha Lusanga, Muheza mkoani Tanga.
TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Kisaka, klabu ya Simba na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Marehemu Kisaka ameacha mjane na watoto wanne. Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe.

Monday, 23 December 2013

BREAKING NEWS: TRESOR MPUTU AMUKIMBIA RASMI SAMATA TP MAZEMBE





Mshambulia hatari wa TP Mazembe imeihama rasmi klabu yake na kukimbilia kwa mabingwa wa Angola timu ya Kabuscorp na kuwacha watanzania wawili Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu kuwa washambuliaji tegemeo kwenye club hiyo tajiri ya Congo taarifa kutoka website ya club hiyoo Mputu ataambulishwa jumamosi ya wiki hii mjini Luanda

PICHA YA SIKU


TAARIFA KUTOKA TFF

Mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya Yanga na Simba iliyochezwa juzi (Desemba 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 imeingiza sh. 422,611,000.
Mapato hayo ni kutokana na washabiki 52,589 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 40,000. Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 19,044.
Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa kutokana na mapato hayo ni sh. 64,466,084.75 wakati gharama za kuchapa tiketi ni sh. 7,488,000.
Mgawo mwingine ilikuwa kama ifuatavyo; kila klabu imepata sh. 117,470,066.61, asilimia 15 ya uwanja ni sh. 52,598,537.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 35,065,691.53 wakati gharama za mchezo zilikuwa sh. 28,052,553.22.
*WAKATI HUO HUO MALINZI, MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa na mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika kesho (Desemba 24 mwaka huu).
Mkutano huo utafanyika saa 6 kamili mchana kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

MESSI, OKWI, NA KASEJA AMUFUKIZISHA KAZI KOCHA YANGA

MUDA mfupi uliopita klabu ya soka ya Yanga imetangaza kusitisha mkataba na kocha wake Ernest Brandts baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, mkataba wa Brandts ambaye ni raia wa Uholanzi umesitishwa rasmi leo hii asubuhi na ameshakabidhiwa barua ya kumtaarifu juu ya hali hiyo.

“Tumesitisha mkataba na kocha wetu na ameshakabidhiwa barua yake, huo ni uamuzi wa uongozi mzima wa Yanga, kila kitu kimeenda sawa katika kuachana naye,” alisema Kizuguto.

Tetesi za Brandts kutimuliwa zilizagaa jijini Dar es Salaam tangu jana muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji kwamba hata kama klabu itaamua kuachana na kocha huyo itafuata taratibu zote.

Uamuzi huo wa Yanga unaonekana pia kuchagizwa zaidi na kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Simba katika mchezo maalum wa kirafiki maarufu kama Nani Mtani Jembe uliochezwa wikiendi iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. ambao Ramadhani Singano Messi ndo alikuwa nyota wa mchezo


Kingine ambacho Brandts amefanya kufukuzwa ni kulalamika wazee wa kazi kusajili wachezaji bila kumuuliza ambao mara kwa mara kocha huyoo alikuwa analalamika usajili wa Kaseja maana alikuwa na magolikipa wawili wazur na alilalama ujio wa Emanuel Okwi maana halikuwa chaguo lake .

Sunday, 22 December 2013

MANJI AWAFARIJI WANA YANGA BAADA YA KIPIGO

Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Bw. Yusuf Manji amewaomba wanachama, wapenzi na washabiki wasivunjike moyo kwa matokeo ya jana ya mchezo wa kirafiki dhidi ya ya Simba SC, mechi iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga makutano ya mitaa wa Twiga/Jangwani Manji amesema anajua wanachama, na wapenzi wameumia sana hakuna aliyefurahishwa na matokeo ya kufungwa mabao 3-1 lakini isiwakatishe tamaa uongozi unafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza.
"Mechi ya jana ilikuwa ni bonanza, ndio maana hapakuwa na timu iliyopata pointi katika mchezo huo zaidi ya kusherehekea, sisi tumepata zawadi ya milion 98 wakati wenzetu Simba SC wamepata milion 1, hivyo zaidi sisi tumeendelea kuimarika kiuchumi zaidi wenzetu wameishia kusherehekea" alisema Manji. 
Aidha amesema wachezaji zaidi ya tisa wa Yanga hawajapata muda wa kupumzika tangu mwezi Novemba baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu kwani walijiungana timu za Taifa na wamekua huko kwa takribani mwezi mzima bila kupumzika tofauti na wenzetu Simba SC ambao hawana wachezaji wengi timu ya Taifa.
Manji pia alisema anawapa hongera timu ya Simba SC kwa kushinda bonanza la jana, amesema mchezo wa jana walicheza vizuri hivyo wanastahili pongezi kwa hilo.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya mapungufu yaliyojitokez katika mchezo wa jana, amesema kamati husika inayafanyia kazi na kwa kuwa yeye anasafiri leo kwenda nje ya nchi  majukumu yote amemkabidhi makamu mwenyekiti Clement Sanga mpaka yeye atakaporejea.

MATUKIO MBALIMBALI MECHI YA GOLOSO FC NA STATISTICS3 SC

FIAR PLAY baada ya mechi
Winga wa statistics Lucky(Nani) akipata huduma ya kwanza mbele Ally (sina mudaa)
USIOMBEEEE mfungaji wa mabao mawili ya GOLOSO Enock (Ozil) mwenye mpira akifanya mavitu yakeee mbele ya Mhere(Domayo) cr
FAIR PLAY baada ya mechi wachezaji, wote wakipiga picha ya pamoja
Beki wa GOLOSO FC Kway Yuda (Vidic) akiangalia mpira
Lukuba(Janujaz) akitafuta mbinu ya kufunga
Mwaipungu(Johnson) akipiga kanzu mtu
Enock maarufu kana Ozil akijaribu kuwatoka viungo wa statistics Stev(Kagawa) kulia na Malibwadu(Gustavo) katikati mwenye jezi ya barcalona
Karim Stev (Kagawa) akichanja mbunga katikati ya dimbaa





Beki la GOLOSO FC Joseph Mwaipungu (Johnson) akikokota mpira mbele ya lucky(nani) kulia na stev(kagawa) kushoto
Winga wa statistics mwaka wa tatu Erick Nkya (Neymar) akitoa upinzani ndani ya goli la GOLOSO FC

Timu ya GOLOSO FC waliosimama kutoka kulia ni Alex, Mwaipungu, Lukuba, Kenedy, Gwaser, Hamis, Enock, Yuda, Rajabu, na Danny, aliyechuchumaa ni golikipa Pitta
Timu ya watakwimu mwaka wa tatu waliosimama kutoka kulia na Rojas, Majenga, Lucky, Stev, Malibwadu, Mrisho, Nkya, Matanga na Ally(sina muda) waliochuchumaa kutoka kulia ni Mhere(cr), Ephata, Sureee na Dutch

Saturday, 21 December 2013

GOLOSO FC WAIFUNGA TIMU YA STATISTICS MWAKA WA TATU MABAO MATATU KWA MOJA

Timu ngumu ya GOLOSO FC leo imeweza kuwafunga timu ya watakwimu mwaka wa tatu mabao matatu kwa moja, mabao ya GOLOSO FC yalifungwa na hamis (1) dak35 na enock(2) dk65 na 73 huku la kufutia machozi la wanastatistics likifungwa na mrishoo(ronadhino)dak 86
VIKOSI VYA LEO
    GOLOSO FC
1)Pitta-Kaseja
2)Mwaipungu-Johnson
3)Gwaser-Evra
4)Yuda-Vidic
5)Danny-Chicharito
6)Enock-Ozil
7)Rajabu-Wilshere
8)Hamis-Carzola
9)Kenedy-Torres
10)Alex-Mata / Dakani-Modric
11)Lukuba-Janujaz
 STATISTICS SC
1)Mrishoo-Ronadhino
2)Mhere-Domayo / Ally
3)Ephata-Sagna
4)Dutch-T.Silva
5)Majenga-Masherano
6)Maribwadu-Gustavo
7)Matanga-Chicarito / Rojas-Dida
8)Stev-Kagawa
9)Suree-Ba
10)Nkya-Neymar
11)Lucky-Nani

BAYAN 2 VS RAJA 0

FC BAYERN MUNCHEN BINGWA WA KOMBE LA DUNIA KWA VILABU 2013

Bayan wakishagilia kombe baada ya kuwafunga Raja Casablanca mabao mawili kwa bila

PICHA YA LEO


SIMBA NDIYE MTANI JEMBE,YAIONESHA SOKA SAFI YANGA, YAICHAPA 3-1

 Wachezaji wa Simba na Yanga wakisalimiana.
Kikosi cha Simba waliosimama kutoka kulia kocha Logarusic, Joseph Owino, Jonas Mkude, Hamis Tambwe, Donard Musoti, Henry Joseph, na kocha msaidizi Seluman Matola waliochuchumaa kutoka kulia ni Issa Rashidy, Awadh Juma, Ivo Mapunda, Haruna Chanongo, Haruna Shamte na Salum Said
 

Kikosi cha Yanga  kutoka kulia waliosimama David Luhende. Haruna Niyonzima, Frank Domayo, Mrisho Ngassa, Mbuyu Twitwe, Kelvin Yondani, Athumain Idi, Hamis Kiiza, Nadir Haroub, na  Kavumbangu aliyeinama na golikipa Juma Kaseja
 
 Benchi la  timu ya Simba.
Benchi la Ufundi la Yanga.
 Henry Joseph wa Simba (kushoto) akichuana na beki wa Yanga, David Luhende.
 Henry Joseph wa Simba (kushoto) akichuana na beki wa Yanga, David Luhende.
 Mashabiki wa Simba wakishangilia bao la kwanza la Hamis Tambwe.
 Raha ya ushindi .
 Furaha kwa Simba.

 Hamisi Kiiza akitafuta mbinu za kumtoka, Ramadhani singano.
 Ivo Mapunda akiruka juu kuokoa moja ya hatari langoni mwake.
 Mashabiki wa Yanga wakiwa hawaamini kilichotokea uwanjani baada ya kuchapwa 3-1 na watani zao wa jadi Simba.
 Juma Kaseja akibembelezwa na Mbuyu Twite baada ya kusababisha goli la tatu
 Mmoja wa mashabiki wa Yanga akitolewa nje baada ya kuzimia uwanjani.
 Emmanuel Okwi akimtoka beki wa Simba.
 Wachezaji wa akiba wa Simba  wakishangilia baada ya filimbi ya mwisho. 
 Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic akishangilia baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa 3-1.
 Wachezaji wa Simba wakimnyanyua juu kocha wao, Zdravko Logarusic mara baada ya kumalizika kwa mchezo maalumu wa Nani Mtani Jembe uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba ilishinda 3-1.




 Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe akimkabidhi kombe nahodha wa Simba Haruna Shamte.
Kapteni wa Simba HARUNA SHAMTE akinyanyua kombe juuuuu

Simba wakifurahi na mwali wao baada ya kumshida Yanga

Baadhi ya bechi la simba na wachezaji Awadhi(16), Shamte(26) Hamud(24) na Berko nyuma Wakipiga picha na kombe