Pages

Thursday, 30 January 2014

MBWANA SAMATA MCHEZAJI BORA WA MWAKA TP MAZEMBE


Mshambuliaji wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka na mashabiki wa klabu yake ya TP Mazembe katika ya mchezaji bora wa mwaka wa klabu hiyo iliyopewa jina la "Corbeau d'Or". Samatta ambaye amepewa jina la utani la "Samagoal" na mashabiki wa TP Mazembe aliwabwaga wachezaji wengine watano waliokuwa wakishindana.

           kura zilikuwa kama ifuatavyo

  1. Mbwana Samatta – Kura 248

  2. Asante Solomon – Kura 219

  3. Robert Kidiaba – Kura 200

  4. Nathan Sinkala – Kura 97

 5. Rainford Kalaba – Kura 67

MSIMAMO WA MOU JUU YA ETO'O CHELSEA



Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amefunguka kuhusu mustakabali wa mshambuliaji wake Samuel Eto'o. Akiulizwa na waandishi wa habari kuwa Eto'o atabaki mwisho wa msimu au ataondoka, Mourinho alisema ' Samuel alipenda mwenyewe kuja Chelsea, aliniambia hajawahi kucheza ligi ya England na angependa kujiunga na Chelsea ili atengeneze historia ya kucheza ligi kuu ya England. Mwisho wa msimu huu atakuwa ameshafanikisha nia yake ya kucheza EPL, sasa... siwezi kujua kama atabaki au ataondoka. Lazima mjue kuwa Eto'o hataki kushinda kombe lolote, hana haja na pesa au kuwa mchezaji bora, anachokifanya sasa hivi ni kufurahia maisha yake kwenye soka. Alisaini mkataba wa mwaka mmoja na nilishamsikia akisema atamalizia historia yake ya soka kwenye klabu iliyomkuza Real Mallorca, kwahivyo mwisho wa msimu huu yeye ndiye ataamua kubaki au kuondoka, lakini mimi ningependa abakie kwasababu anatusaidia sana kama timu'. Eto'o mwenye umri wa miaka 34 ameshashinda vikombe vyote vya ligi za Italia na Hispania, alishawahi kuwa mchezaji bora wa Afrika na alishawahi kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani.

Sunday, 26 January 2014

INTER BLOCKS CUP YAFIKIA TAMATI

THE CHAMPION OF INTER BLOCKS CUP
IS
BLOCK (RRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRR)

Mashidano ya inter blocks cup imefikia tamati katika viunga vya COED udom  kwa vijana kutoka kijijini (ujasi) BLOCK(R) kuwa mabingwa wa kwanza wa michuano hii kwa kuwafunga watoto wa mwarabu BLOCK(H) kwa penaty (4 kwa 3)
ZAWADI(MBUZI)


WASHIDI WA INTER BLOCKS CUP
MSHIDI WA KWANZA 
-Block (R)
-zawadi mbuzi watatu na kombe

MASAI KAPTENI WA BLOCK (R) AKISALIMIANA NA MGENI RASMI ILI KUPEWA KOMBE LAO

MSHIDI WA PILI
-Block (H)
-zawadi mbuzi mmoja na cret moja
GERRAD AKIPOKEA MPUNGA NA MBUZI WAO

MSHIDI WA TATU
-Block (I)
-zawadi cret mbili za soda
KITARIMA KAPTENI WA BLOCK(I) AKIPOKEA MPUNGA WA MSHIDI WA TATU


WASHIDI KWA AKINA DADA

MSHIDI WA KWANZA
-Kombaini ya Block (A,D&K)
-zawadi mbuzi moja na kombe
MARIAM AKIKABIDHIWA KOMBE NA MGENI RASIMI


MSHIDI WA PILI
-Kombaini ya block(L,N,&O)
-zawadi cret mbili za soda


TUZO MBALI MBALI KATIKA MICHUANO HII

MCHEZAJI BORA WA MICHUANO
-beki kutoka block(H)
-zawadi jezi orginal
BEKI KISIKI LA BLOCK(H) wa pili kutoka kushoto ndio MCHEZAJI BORA


MFUNGAJI BORA
-Danny
-mabao sita(6)
-mshambuliaji kutoka block(H)
-zawadi jezi orginal


MCHEZAJI MWENYE NIDHAMU
-Kitarima robert
-kapteni kutoka block (I)
-zawadi jezi orginal



KAPTENI BORA WA MICHUANO
-Steven Karim
-kapteni kutoka block(E)
-zawadi jezi orginal


GOLIKIPA BORA
-kutoka block (I)
-zawadi jezi orginal


GOLI BORA
-Sekenja Mwenga
-mshambuliaji kutoka block(H)
-goli kati ya block(F) vs block (H) nusu fainali
-zawadi jezi orginal


MCHEZAJI BORA KWA AKINA DADA
-Mariam
- kapteni wa kombaini ya block (A,D,&K)
-zawadi jezi orginal



MATUKIO MBALI MBALI YA MECHI ZA LEO
KIKOSI CHA KOMBAINI YA BLOCK(A,D,&K)

KIKOSI CHA KOMBAINI YA BLOCK(L,N,&O)

. MGENI RASIMI AMBAYE NI RAISI WA KITIVO CHA ELIMU UDOM

MARIAM AKIIFUNGIA TIMU YAKE BAO KWA NJIA YA PENATI

KAPTENI WA KOMBAINI YA BLOCK(L,N&O) AKIWA KAZINI

MABINGWAAAAAA BLOCK(R)

RAISI MWAMBENE  IKIWA MEZA KUU NA MAKOMBE

JAMAA ALIKUWEPO KUWAPA SAPOTI BLOCK(R)

KILICHOWAKOSESHA KOMBE BLOCK(H) NI HIKI ALIWAKUWA WAMEJITANGAZA MABINGWA KABLA YA MECHI IKAWA KINYUME CHAKEEE

WANAUMATI WALIKUWEPO KUGAWA KONDOMU UWANJANI

MWANAGOLOSO MOLLA JEROME WA KWANZA KUSHOTO IKIWA NA BOX LA WANAUMATI


BLOCK(R) WAKISHAGILIA

FURAHA NA MWARI JUUUUUUUU


KAPTENI WA BLOCK(H) AKILIA BAADA YA MECHI AKIWA NA MENEJA WA TIMU YAKE

MASHABIKI NAO WALIFURIKA






Friday, 24 January 2014

RATIBA LIGI KUU TANZANIA WEKENDI HII

JUMAMOSI TAR:25-JANUARY-2014
    
1)ASHATI VS YANGA
  uwanja: taifa Dar es salaam

2)AZAM VS MTIBWA SUGAR
 uwanja: chamazi comlex Dar

3) COASTAL UNION VS OLJORO JKT
uwanja: mkwakwani Tanga

4)KAGERA SUGAR VS MBEYA CITY
uwanja:kaitaba Kagera


JUMAPILI TAR:26-JANUARY-2014

1)SIMBA VS RHINO RANGERS
uwanja: taifa Dar

2)JKT RUVU VS MGAMBO SHOOTING
uwanja: azam complex Dar

Thursday, 23 January 2014

MOHAMED SALAH ATUA CHELSEA



Klabu ya Chelsea imeipiku klabu ya Liverpool kwa kumsajili mshambuliaji wa FC Basel, Mohamed Salah maarufu kama messi wa misri kwa paundi mil 11. Mshambuliaji huyu tayari alikuwa kwenye hatua za mwisho kujiunga na klabu ya Liverpool na alikwenda jijini Liverpool kukutana wa viongozi wa klabu ili kumalizia makubaliano ya malipo yake. Makubaliano baina ya Liverpool na FC Basel yamechukua muda kutokana na kutokukubaliana kuhusu ada ya uhamisho. Klabu ya FC Basel ilikuwa ikihitaji paundi mil 12 wakati klabu ya Liverpool ilikuwa tayari kulipa paundi mil 5 hadi 8. Mvutano huu baina ya Liverpool na FC Basel ndiyo uliyoipa mwanya klabu ya Chelsea kumnasa Salah kutoka mikononi mwa Liverpool baada ya kuchukua paundi mil 37 kutoka man united kwa mauzo ya Juan Mata boss wa chelsea hakufanya kosa ambapo aliweza kuwanyang`anya livepool mikononi si mara ya kwanza kwa clabu ya chelsea kupora wachezaji kutoka timu mbalimbali chini ya mou aliweza kuwafanyia hivyo man u kwa mikel obbi akiwa uwanja wa ndenge, pia tottenham walikuwa na uhakika kwa asilimia 99 wamemupata Willian ila dakika za mwisho mou akamchomoa, ndicho kilichotokea kwa liverpool

                       
                           GOLOSO LA SOKA

                             Na Yossima Sitta & yudathadei kway     

    SOKA KATIKA UHALISIA WAKE

Swali likiulizwa, Je ni mchezo gani maarufu zaidi duniani? Bado linabaki kuwa swali lenye utata kwa maana ya kwamba umaarufu kimchezo unaweza kuwa ;mchezo unaoangaliwa na wadau walio wengi kwa maana ya kuamasika na mchezo husika au inaweza kuwa mchezo uliochezwa kwa muda mrefu zaidi duniani au unaweza kuwa mchezo wenye kuingiza mapato zaidi duniani. Katika kulitazama hili la mchezo wenye hamasa zaidi duniani kwa kuangaliwa na kufuatiliwa na walio wengi, tafiti za kina zimefanyika kimataifa na imebainika kuwa  watu wapatao 3.3-3.5 bilioni kutoka katika mabara mbalimbali (Ulaya,Africa, Asia ,Americas ,n.k) ni wakereketwa wa mchezo wa soka, mpira wa miguu. Takwimu hizi ni kati ya jumla ya watu wanao kadiriwa kufikia billion 7.137 Dunia nzima kulingana na taarifa iliotolewa na United States Census Bureau (USCB ) hapo 12,March,2012. Tukiingia ndani zaidi  kitafiti inaonyesha  mchezo huu unakadiriwa kuchezwa na wachezaji million 250 katika nchi zipatazo 200 na kudhihirisha kuwa mchezo maarufu zaidi katika sayari hii. Michezo inayofuata kwa umashuhuri ni pamoja na Cricket wenye wakereketwa wapatao 2-3 billion. Field Hockey wenye mashabiki wanaofikia 2-2.2 billion na mchezo huu ni maarufu zaidi katika nchi za Asia, Ulaya, Australia, n.k ukifuatiwa na Tennis mchezo wenye mashabiki wapatao billion 1 zaidi katika nchi za Ulaya, Americas na Asia.
Katika kujikita kisoka zaidi kuna sababu nyingi zinazo jaribu kuthibitisha ni kitu gani kinachofanya mpaka watu kuvutiwa na mchezo huu zaidi na hata wengi wao kudiriki kukiri ya kuwa hawana sababu maalumu isipokuwa wamejikuta wakiupenda tu. Hili liko wazi hata kwa wale walio na uzoefu kama sio professionals katika uliwengu wa mapenzi mtu akimpenda mwenzi wake basi kama sio kwa sababu za tamaa tamaa tu, Huwa ni ngumu  kuwa na sababu ya moja kwa moja  iliomfanya au inayomfanya kumpenda mwenzi wake zaidi inabaki kuwa ni uhalisia usio elezeka kirahisi. Hii ndio sababu nzito zaidi kwa walio wengi katika upenzi wa mchezo huu tajwa.Tumepata kusikia matukio mengi yanayoendana na upenzi katika tasnia hii ya soka, Kama vile watu kujiua kisa timu zao kufungwa, mashabiki kuuawa kisa tu mashabiki kuwa wengi kuliko ukubwa wa uwanja. Watu kucheza kamari na hata kujivunia mengi yaliyo ya thamani na hata wengine kusadikika kuwaweka wake zao rehani kisa tu ni upenzi uliokithiri juu ya mchezo huu mashuhuri zaidi. Lakini kupitia mchezo huu vijana wengi wanajipatia ajira tena zenye ujira wenye kuridhisha kabisa na zaidi ni nchi nyingi kufaidika kiuchumi kupita mchezo huu kama vile kwanjia ya michuano mbalimbali inayowaleta pamoja katika eneo moja umati wa watu kutoka maeneo mbalimbali nje na eneo husika.
 Mengi yanafanyika katika harakati za kuufanya mchezo huu kuwa bora kila kukicha, baadhi ya mambo yaliofanyika kupitia mashirikisho ya soka duniani ni pamoja na kuanzisha soka la wanawake na hata kufikia hatua ya kombe la dunia la wanawake na hivyo kutanua wigo, nikimaanisha hapo kabla mchezo huu ulikuwa ukiwahusisha wanaume tu lakini sasa hata wanawake wanajikakamua kwenye pitch. Bila kusahau Shirikisho la mpira wa miguu ulaya(UEFA) kuboresha maamuzi uwanjani kwa kuweka vibendera wanne mmoja kwa kila upande wa pitch. Bila kusahau shirikisho la soka la Uingereza(FA) kuanzisha teknolojia ya goli katika kutambua goli kama ni halali au la.
Jitihada pia zinafanyika katika ngazi za vilabu ikiaminika ya kuwa ubora wa mpira katika timu za taifa unachangiwa zaidi na nguvu kubwa katika vilabu. Katika soka imani ziko nyingi lakini zaidi ninalotaka kuligusia katika kipengele hiki ni wimbi la kuwaamini walioishakuwa wachezaji kuwa mameneja katika timu mbalimbali. Jambo hili linatafsiriwa na wanamichezo kama jambo lenye tija zaidi katika kuleta ladha kamili kisoka kwani meneja aliyeisha kuwa mchezaji ni wazi ya kwamba anatambua ni nini kifanyike uwanjani na nani na katika muda gani na mwisho wa siku kutarajia matokeo mazuri.
Haya yameshuhudiwa na watabe  waliowika enzi hizo na mwisho wa siku kukabidhiwa mikoba ya ukocha.  Baadhi wakiwemo Frank Rijkad aliekuwa akiifundisha Barcelona na hata kufanya makubwa akiwa na masupa staa kama Ronaldinho Gaucho na Samwel Eto’o, Akaja  Pep Gaudiola  aliyekuwa kiungo mkabaji kipindi cha enzi zake na baadae kuwa kocha katika timu ya Barcelona B baadae Barcelona ya wakubwa kuanzia mwaka 2008-2012. Ambapo katika kipindi hicho alifanya maajabu katika tasnia ya soka la vilabu na baadae katika msimu huu kupewa mikoba ya kuinoa klabu mashuhuri duniani  inayosifika kwa  mpira wenye hekima nikimaanisha ina wachezaji wenye sifa za kucheza mpira wenye kasi, nguvu na umakini katika kupiga pasi na kufunga hawa ni Bayern munich mabingwa watetezi wa kombe la UEFA. Wako makocha wengi walio aminiwa na kupewa majukumu hayo na walishafanya makubwa kwenye pitch wakiwemo Meki Mexime ‘’kaptani’’ Seleman Matola, Dunga, Diego Maradona na wengine wengi. Katika wiki hii tumeshuhudia pia klabu ya Ac Milan ikifanya maamuzi mazito kwa kumfukuza aliye kuwa kocha wake Massimiliano Allegri na kumkabidhi mikoba kiungo wa timu hiyo ambaye alikaa kwa kipindi cha miaka kumi mdachi Clarence Seedorf. Yamesemwa mengi na walio wengi na  wengi wao wakitegemea makubwa katika klabu hio iliyokuwa na mwanzo mbaya katika ligi kuu ya Italia maarufu kwa Serie A.
Hizi zooooote ni mbwembwe za soka mchezo unaosadikika kuanza kuchezwa katika nchi ya China (karne ya 2 na 3 Kabla ya Kristu) na kusemekana ya kuwa waingereza ndio walio boresha mchezo huu kama tunavyo uona hivi leo. Soka ndiyo habari ya mjini na vijijini, mashuleni na vyuoni, watoto, vijana, rika la kati na hata wazee Kuongelea soka kila siku.

          waandishi wa makala hii 

Yossima Sitta (mhariri & afisa habari wa goloso)
Yudathadei Kway (msanifu wa habari za kimataifa wa   goloso)

This is how Wenger respond towards Mata transfer to United

Mata move will not be Manchester United's 'Ozil moment' - it is just the beginning

manager Arsene Wenger believes Juan Mata's proposed move from Chelsea to Manchester United is unfair and feels the rules of the transfer window should be adapted.


The Frenchman is annoyed that the two clubs involved in the transfer do not have to play each other again this season, but that United will still meet the Blues' title challengers - Liverpool, Manchester City and the Gunners - with Mata in their ranks.

United have prepared a temporary helipad at Carrington as the Spaniard flies in to complete a £37 million club record transfer on Thursday, but Wenger believes the timing is wrong.

"It opens again a little bit the opportunity of this transfer market because Chelsea had already played twice against Man United so they don't play again," he told reporters.

"They could have sold him last week but it opens at least the opportunity [to question] the dates of this transfer window.

"Some teams have already played twice against one opponent and some others not. I think if you want to respect the fairness for everybody exactly the same, that should not happen.

"I just think you would want that everybody is on the same level. Chelsea do not make the rules but maybe the rules should be a bit more adapted to more fairness."

Wenger, who sold Robin van Persie to Manchester United in 2012, is puzzled by the Mata move.

"I am surprised because Juan Mata is a great player and Chelsea sell a great player to a direct opponent," he continued.

Wenger also backed David Moyes to ride out United's rough patch, after the club were knocked out of the Capital One Cup semi-finals by Sunderland on Thursday.
"You have to survive massive disappointments and keep your belief high in what you do because to win is easy for everybody," he added.
"How to live with defeat, that is what managers are about, and David Moyes is strong enough. For me he deals with the situation very well.
"They go through a difficult moment in their season but they can still come back. They are in a strong position in the Champions League and they just bought a great player, so Man United has still to be considered a threat."

Wednesday, 22 January 2014

ABDUUUUUUUUL GOOLOOOOOOOSOOOOOOO ( BLOCK (I) WAKAAAAAAAA)

INTER- BLOCK CUP BLOCK (R) NAO WATINGA FAINAILI
-Vijana kutoka kijijini  BLOCK(R) wametinga fainali baada ya kuwafunga WASAFI vijana kutoka mjini mtaa wa pili BLOCK (I) kwa goloso moja kwa bila lililofungwa dak:88 na Abdul

FAINALI
YA WANAUME
 BLOCK(H) VS BLOCK (R)

YA WANAWAKE
KOMBAINI ZA
BLOCK(A,D,K) VS BLOCK (L,N,O)

MSHINDI WA TATU
BLOCK (F) VS BLOCK (I)

WAFUNGAJI
5- Danny (block H)
4-masai (block R)
3-mwenga (block H)
  -alex (block M)
  -enock (block E)
  -ibrahim (block F)


MATUKIO YA MECHI YA BLOCK(I) VS BLOCK(R)
ABDUL MFUNGAJI WA BAO PEKEE LA BLOCK (R)

MASAI AKIPIGA GOLI KIKI

REFA WA MECHI YA LEO AKITETA JAMBO NA KAMISAA WA MECHI



KOCHA WA BLOCK (R)

MROPEEEE KAZINI

KOCHA WA BLOCK (I) AKITOA MAELEKEZO KWA WACHEZAJI WAKE MAJENGA, SANDEE NA MRISHOO

KOCHA MSAIDIZI WA BLOCK (R)



FURAHA BAADA YA MECHI




Tuesday, 21 January 2014

WATOTO WA MWARABU HAOOOOOOOOOOOOOO FAINALI

MATOKEO
 BLOCK (F) 2 VS BLOCK(H) 4
wafungaji
block(F)
(joseph dak:30 ibrahim dak:88)
block (H)
(mwenga dak:14 danny dak:22,70 meshack dak:50)

MATUKIO YA MECHI YA LEO

TIMU ZIKIPATA MAELEKEZO KUTOKA KWA WAANDAAJI

MWENGA MFUNGAJI WA BAO LA KWANZA LA BLOCK(H)

DANNY  MFUNGAJI WA MABAO MAWILI YA TIMU YA  BLOCK(H)

BLOCK(H) WAKISHAGILIA BAO LA PILI


JOSSEPH MFUNGAJI WA BAO LA KWANZA LA BLOCK (F)

MPIRA FITINA: HUYU NI KOCHA WA BLOCK (I) (mwenye shati jeupe) AKITOA MAELEKEZO KWA CAPTENI WA TIMU YA BLOCK(H)

FITINA FITINA: CAPTENI WA TIMU YA BLOCK(E)  NAYE HAKUWA NYUMA KUWAPA HAMASA VIJANA WA BLOCK(F)

MESHACK MFUNGAJI WA BAO LA TATU

SAM AKIMPONGEZA MECHACK KWA BAO ZURI

CHEZEA DANNY (EMMANUEL GOLOTA) AKISHAGILIA BAO LA TATU

IBRAHIM MFUNGAJI WA BAO LA PILI LA BLOCK(F)