GOLOSO LA SPORT
NA YOSSIMA SITTA
Nchi yetu haikosi
vitimbwi kila kukicha unafiki unafiki, majungu majungu kila sehemu na kila
secta hapa nchini achana na unafiki unaofanya kwenye maofisi ya serikali na
yale ya umma maana bila kujuana utasubili sana, Achana na unafiki unaoendelea
ndani ya chama cha Chadema na Zitto wao, Pia futa unafiki wa Diamond na mademu
zake, Kila sehemu unafiki na majungu ndo habari ya mjini angalia Tff wanavyofanya
kazi kifitina kuwapata viongozi wao. Usiombe kukutana na fitina za Ccm kwenye
siasa za bongo lakini haya ndio maisha yetu kwa sasa mpaka sasa siasa, majungu,
fitina zimeingia kwenye soka letu la Tanzania kila mtu anaamua tu anachokiamini.
Kocha mkuu wa timu ya Yanga
Ernest Brandts amepewa notice ya mwezi mmoja ataamua mwenyewe kama ataendelea
kuifundisha yanga ndani ya mwezi mmoja au lah, Sioni mantiki ya kufukuzwa kwa Brandts
wazee wa kazi wamesema sababu ya kupewa notice ya mwezi mmoja ni kwa sababu ya
kutoridhishwa na kiwango cha uchezaji wa timu yao kwenye baadhi ya mechi na
mechi ya bonanza kama wanavyoita wao yaani mechi ya mtani jembe dhidi ya watani
wao wa jadi Simba ambayo ilichezwa katika uwanja wa taifa na kuambulia kipigo
cha mabao matatu kwa moja
Uongozi wa Yanga
umefanya fitina na ili kumfukuza kazi kocha wao Ernest Brandts mengi yamesemwa
na mengine yanaendelea kuibuliwa eti amefukunzwa kwa sababu timu imekosa
ufanisi, Kutoridhishwa kwa uchezaji wa timu nzima, Kufungwa na Simba mechi ya
mtani jembee, Kikosi kuwa na mastaa wengi na kushindwa kuifunga Simba yenye
watoto wengi, ila yote yatasemwa na watu wataendelea kusema ila kilichomfukuzisha
kazi kocha wa Yanga ni Emmanuel Okwi na Juma Kaseja Juma kwa nini nasema Okwi
na Kaseja wamemfukuza Brendts ni kwa sababu wamesajiliwa kwa matakwa ya uongozi
na si kwa mahitaji ya kocha
Huwa nazishagaa sana
vilabu vyetu hasa Simba na Yanga usajili wa wachezaji huwa unafanya na viongozi
na si bechi la ufundi angalia wazee wa kazi ndani ya Yanga wanavyosajili
wachezaji si kwa mahitaji ya kocha bali ni kwa mahitaji ya kuwaridhisha
mashabiki wao wa Yanga na kuikomoa
Simba. Ujio wa Kaseja na Okwi Yanga ni wa kishabiki zaidi na kuikomoa Simba
kitu ambacho ni hatari kwa kilabu utaifunga vipi Zamarek ya Misri, Enyimba
na Tp Mazembe kwenye ligi ya mabingwa
kama unasajili kishabiki zaidi, Wazee wa kazi Seaf Magari, Bin Kaleb, na Mutabara
wanamwaga pesa ili kuwafurahisha mashabiki wao si wanajua mwana mkubwa Yusuf Manji amesema hatangombea tena nafasi ya
mwenyekiti wanaweza kuichukua Yanga hapo mbeleni. Wanafanya hivyo ili kuteka
hisia za wapenzi na mashabibiki wa Yanga maana walishajua watanzania sisi ni
wazembe wa kufikiria na kuangalia mbali leo Yanga wanashagilia uwepo wa Okwi na
Kaseja na kusahau kabisa kwenda kumuuliza ahadi hata mbili tu Manji
alizowaahidi wakati anaomba kura kuwa rais wa kilabu yaooo
Kila mara nilikuwa
namsikiliza kocha Brandts akikataa usajili wa Kaseja maana tayari alikuwa na
makipa wawili wazuri wenye hadhi ya kimataifa Ally Mustafa Bathez na Deo
Munishi Dida sasa Kaseja Juma anakuja kufanya nini? kwa sababu ni chaguo la
bossi wako lazima ukubali kuwa naye na ukikubali kuwa naye tena inakulazima
umpange kwenye kikosi cha kwanza ili mashabiki wafurahi na wazee wa kazi
waonekane wamefanya kazi ya maana la sivyo wakufute kazi ndio utamaduni wetu
kwa soka letu na siasa nyingi sana. Pia kama vile timbwili lanaelekea ukingoni
Brandts tena akasikia wazee wa kazi wamemalizana na Okwi, sina tatizo na
kiwango cha Emmanuel Okwi na kocha yoyote atakuwa tayari kufanya kazi na okwi
ila kumletea okwi matakwa ya mashabiki wao ndio alichokuwa analalama kocha
maana yanga ilikuwa na viungo na winga wazuri ngassa, Msuva, Niyonzima, Chuji,
Nizar, Domayo, sasa Okwi wa nini bora kidogo usajili wa kinda Shaaban dilunga.
Vilabu nyetu vimekosa
mipango na uvumilivu kabisa hasa Simba na Yanga sijaona kocha anamaliza hata
miaka sita kuwa kwenye bechi la ufundi. Wamekuja wengi wamefukuzwa wengi si kwa
sababu ya ufundi ni kwa sababu ya unafaiki au kufungwa Simba au Yanga poleee
Brandts hizi ni siasa za soka letu lakini wewe ni Professional na utabaki kuwa
Professional tu.
0769-183981
0 comments:
Post a Comment