Pages

Friday, 10 January 2014

INTER-BLOCK LEO BLOCK(S) 2 VS BLOCK (J) 2

Mpira ulianza kwa kasi kila timu zikishambuliana kwa kutegeana ila vijana wa BLOCK (J) walikuwa wazuri maana walikuwa wanamiliki mpira vizuri kuliko wachezaji wa timu ya masters BLOCK (S) haikuwachukua muda vijana wadogowadogo wa block J kupata bao la kuongoza mnamo dak ya 23 kwa faulo iliyoingia moja kwa moja langoni. mpaka mapumziko BOLCK (J) walikuwa wanaongoza kwa bao moja kwa bila
kipindi cha pili kilianza kwa kasi kila timu ikitumia mbinu waliopewa na makocha wao ila muda si punde beki kitasa maarufu kama FUSSO(bonge) aliweza kuisawazishia timu yake ya block (s) bao  kwa faulo. vijana wa wa block (j) walizidi kuchanganyikiwa kwa  kandanda safi  lilikuwa linatandazwa kwenye pitch na wazee wa masters ila baada ya timu kufanya mabadiliko ya wachezaji. mpira uliendelea kwa kasi huku block(s) wakionekana mafundi zaid ambao walikuwa hawana pumzi ya kuzunguka ndimba lotekatika viwanja vya COED, ilitokea piga ni kupige ndai ya 18 ya block S ambapo kijana fundi mwenye kipaji cha hali ya juu akaweza kuipatia timu yake bao la kuongoza  kwa kichwa, ikiwa watu walishakata tamaa kuwa mechi itaisha kwa mabao 2-1 mshambuliaji mrefu kariba ya akina shikokoti aliyetokea bechi maarufu kama COROUCH mnamo dak ya 85 aliweza kuwanyanyua mashabiki wa timu ya masters  kwa kuisawazishia timu yake bao. hadi mwisho wa mpira
        BLOCK(S) 2 VS BLOCK(J) 2
KIKOSI CHA TIMU YA BLOCK(S) masters

KIKOSI CHA TIMU YA BLOCK (J)

0 comments:

Post a Comment