Pages

Thursday, 30 January 2014

MSIMAMO WA MOU JUU YA ETO'O CHELSEA



Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amefunguka kuhusu mustakabali wa mshambuliaji wake Samuel Eto'o. Akiulizwa na waandishi wa habari kuwa Eto'o atabaki mwisho wa msimu au ataondoka, Mourinho alisema ' Samuel alipenda mwenyewe kuja Chelsea, aliniambia hajawahi kucheza ligi ya England na angependa kujiunga na Chelsea ili atengeneze historia ya kucheza ligi kuu ya England. Mwisho wa msimu huu atakuwa ameshafanikisha nia yake ya kucheza EPL, sasa... siwezi kujua kama atabaki au ataondoka. Lazima mjue kuwa Eto'o hataki kushinda kombe lolote, hana haja na pesa au kuwa mchezaji bora, anachokifanya sasa hivi ni kufurahia maisha yake kwenye soka. Alisaini mkataba wa mwaka mmoja na nilishamsikia akisema atamalizia historia yake ya soka kwenye klabu iliyomkuza Real Mallorca, kwahivyo mwisho wa msimu huu yeye ndiye ataamua kubaki au kuondoka, lakini mimi ningependa abakie kwasababu anatusaidia sana kama timu'. Eto'o mwenye umri wa miaka 34 ameshashinda vikombe vyote vya ligi za Italia na Hispania, alishawahi kuwa mchezaji bora wa Afrika na alishawahi kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani.

0 comments:

Post a Comment