GOLOSO LA SOKA
Na Goloso members
Inter blocks cup
MABLOCK YOTE
YADHIBITISHA KUSHIRIKA
Waandaaji waliandaa
form na kanuni pamoja na sheria za mashidano na kuwapa washiriki wote wa
michuano hii timu zote kumi na mbili(12)
yaani Block E, F, G , F, H , I , J, M,
Q, R, S, na T. ila kwa kuwa hii michuano
ilikuwa imelenga kitivo cha elimu timu za block E, F, na J walitoa viingilio
kwa sababu wakazi wao wengi si waalimu mfano block(E) wanakaa wanafunzi wa kitivo cha sayansi asilia na mahesabu,
block (F) wanakaa kitivo cha afya huku block(J) wakazi wengi wanatoka kitivo
cha earth science huku block zingine zikiwa na walimu wengi si hivyo tu bali block
(G, H, I, na J) ikiwa na vijana wa kutoka kitivo cha sayansi asilia na mahesabu
HATUA YA MTOANO YAMALIZIKA
Timu kumi na mbili
zilipangwa kuanzia hatua ya mtoano kufuzu kwenda hatua ya pili ya makundi
waandaaji walichezesha droo kuona nani anapangwa na nani. Wawakilishi wa kila timu
kutoka kila block walihudhuria sherehe hiyo ya upangaji wa timu hatua ya mtoano
na kupangwa kama ifuatavyo
Block(E) vs Block (T)
Block(F)
vs Block (P)
Block
(G) vs Block (I)
Block(J)
vs block (S)
Block (H) vs Block (M)
Block (Q) vs Block (R)
Timu zilicheza mechi
mbili mbili nyumbani na ugenini na timu za block (E, F, H, I, J na R) zilifuzu hatua
ya pili ya makundi kwa jumla ya mabao kama ilivyooneshwa hapo chini kwenye mabano
Block(E) vs Block(T)----(5 vs 2)
Block(F) vs Block(P)---(4 vs 2)
Block(G) vs Block(I)---(1 vs 2)
Block(J) vs Block(S)----(2 vs 2) J
walifuzu kwa bao la ugenini
Block(H) vs Block(M)---(4 vs 3)
Block(Q) vs Block(R)----(1 vs 5)
MAKUNDI YAPANGA NA MECHI ZIKACHEZWA
Baada ya mechi ya
mwisho ya mtoano kati ya block(H) vs block(M) kamati ya mashindano chini ya
mrope na Michael ilipanga makundi mawili
A na B ikiwa kundi A likiwa na timu za
block ( E, H na R) Huku kundi B likiwa
na timu za Block (F, I na J) timu zote
zilicheza mechi mbili mbili kwa kila kundi timu za block (H na R)
zikifuzu hatua ya nusu fainali kutoka kundi A huku wababe block(I na F ) kutoka
kundi la B nao walifuzu hatua ya nusu fainali kama inavyooneshwa hapo chini
Group A
P
W D L F A GD Pts
BLOCK(H) 2 2 0 0 5 2 3
6
BLOCK(R) 2 1
0 1 3 4 -1 3
BLOCK(E) 2
0 0 2 2 4 -2 0
Group B
P
W D L F A GD
Pts
BLOCK(I) 2 1 1
0 2 1
1 4
BLOCK(F) 2 0
2 0 2
2 0 2
BLOCK(J) 2 0 1
1 1 2 -1 1
UDHAIFU WA MICHUANO
Waaandaji walishidwa
kuweka kanuni ambayo ingeweza kufanya michuano hii kuwa mizuri mfano unakuta
refa au kamisaa wanakuwa na timu ambazo wanazisapoti au kuwa kocha wa timu
furani kitu ambacho ni hatari katika michuano hii maana refa anaweza kuchezesha ovyo ili
kuikwepesha timu yake isicheze na timu furani hatua inayofuat .
Kati ya timu ambazo zimeingia hatua ya nusu fainali block (F,H,I, na R) timu za
block R kocha wao ndio refa na kamisaa wa michuano hii, block H muuandaji wa
michuano hii ndio kocha mchezaji wa timu yake, block I wanakamati wa michuano
hii mmoja ndio kocha wa timu ya block(I) na mfadhiri wa timu yao ndio mjumbe wa
kamati ya maandalizi kitu ambacho ni hatari sana katika michuano hii.
MJINI NA VIJIJINI
Kwa ambao hawajui katika
michuano timu zilikuwa na chagamoto timu kutoka kijijni na mjini timu za mjini
zilikuwa hatari sana kwa timu ambazo
zimetoka kijijini kati ya timu 12 timu 6 zilikuwa zinatoka kijijini na 6
zilikuwa zinatoka mjini kati ya timu zilizovuka hatua ya mtoano timu 5 kati ya
6 kutoka mjini zilifuzu hatua ya makundi na timu moja kutoka kijijini nayo
ilivuka hatua ya makundi hiyo ilikuwa imeonesha ni kwa namna gani timu za mjini
zilikuwa vizuri sana kuliko timu za kijijini.
FITINA FITINA
Timu nzima ya
goloso iliweza kuhudhuria mechi zote
mwanzo wa michuano mpaka hatua ya mtoano inamalizika kulikuwa na fitina fitina
mwanzo wa michuano hadi hatua hii ya nusu fainali waandaji na marefa kulikuwa
na timu ambazo walikuwa wanaziombea
zitoke mwazo wa michuano timu hizo ni block(E) (F) na J unajua kwa sababu gan? eti wakazi
wa block hizo tajwa hawatoki katika kitivo cha elimu. Ilidhihirika pale mechi
ya makundi block(E) vs block(R) ambapo waandaji na wanakamati wote walikuwa wanalisapoti
bechi la block (r) kutoa maoni nini kifanyikeee ili waitoe block E ama refa
kumpa mawaidha afanye nini kitu ambacho ni hatari tena sana vijana kutoka
kariakoo watoto wa madukani block E ama nusura watie mpira kwapani baada ya
refa kuonesha mapenzi kwa timu ya block R, mpira ulisimama kwa dak kama 10 timu
zikibishana baada ya refa kuamua penati ipingwe kuelekea katika lango la timu
ya block(E)
GOLOSO TUNAMULIKA MBALI
Timu nzima ya goloso
ilikuwa inachambua mechi mwanzo wa mechi hadi wa mwisho ilikuwa inaongozwa na
mwenyekiti ATTU GERVAS, katibu wa goloso RAJABU JUMA, afisa habari na Mhariri wa goloso YOSSIMA
SITTA, wasanifu wa habari za
kimataifa wa goloso KWAY YUDATHAEI NA
ERICK GWAKISA na wajumbee NGULLY ALEX, LUKUBA ENDREW, MOLLA JEROME,
DANNY JUSTINE, JOSEPH MWAIPUNGU, MASALU,
ENOCK NA HAMISI
ENDELEA KUFUATILIA WWW.GOLOSOLETU.BLOGSPOT.COM
HATUA YA NUSU FAINALI
0 comments:
Post a Comment