![]() |
Klabu ya Chelsea imeipiku klabu ya Liverpool kwa kumsajili mshambuliaji wa FC Basel, Mohamed Salah maarufu kama messi wa misri kwa paundi mil 11. Mshambuliaji huyu tayari alikuwa kwenye hatua za mwisho kujiunga na klabu ya Liverpool na alikwenda jijini Liverpool kukutana wa viongozi wa klabu ili kumalizia makubaliano ya malipo yake. Makubaliano baina ya Liverpool na FC Basel yamechukua muda kutokana na kutokukubaliana kuhusu ada ya uhamisho. Klabu ya FC Basel ilikuwa ikihitaji paundi mil 12 wakati klabu ya Liverpool ilikuwa tayari kulipa paundi mil 5 hadi 8. Mvutano huu baina ya Liverpool na FC Basel ndiyo uliyoipa mwanya klabu ya Chelsea kumnasa Salah kutoka mikononi mwa Liverpool baada ya kuchukua paundi mil 37 kutoka man united kwa mauzo ya Juan Mata boss wa chelsea hakufanya kosa ambapo aliweza kuwanyang`anya livepool mikononi si mara ya kwanza kwa clabu ya chelsea kupora wachezaji kutoka timu mbalimbali chini ya mou aliweza kuwafanyia hivyo man u kwa mikel obbi akiwa uwanja wa ndenge, pia tottenham walikuwa na uhakika kwa asilimia 99 wamemupata Willian ila dakika za mwisho mou akamchomoa, ndicho kilichotokea kwa liverpool
0 comments:
Post a Comment